Home » » MAMA,MTOTO WAFA KWA RADI MPANDA

MAMA,MTOTO WAFA KWA RADI MPANDA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MAMA na mtoto wake, wakazi wa Kijiji  cha Mnyagala,  Tarafa ya Kabungu, Wilaya ya Mpanda, mkoani Katavi, wamefariki dunia baada ya kupigwa na radi wakiwa njiani  kuelekea nyumbani kwao.
Waliokufa wametajwa kuwa ni Migu Samwel (46) na mwanae Nsungulwa Kasanzu (15).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, alisema tukio hilo  lilitokea  juzi saa 12 jioni kijijini hapo.
Alisema kabla ya vifo hivyo mama huyo na mwanae walikuwa  wamekwenda kwa jirani yao kumsalimia na walipoona dalili za mvua waliaga kabla mvua haijaanza kunyesha.
Alisema walipofika jirani na nyumba yao umbali wa mita 15 ndipo walipopigwa  na radi  na kufariki dunia papo hapo. Mama  alipigwa  na radi sehemu  ya kifuani na  mwanae  alipigwa na  radi   sehemu ya kichwani.
Miili ya  marehemu  hao ilitarajiwa  kuzikwa  jana  kijijini hapo  baada ya  taratibu za kidaktari  kukamilika.
Wakati huohuo, Paulina  David (3), mkazi  wa Kijiji  cha  Sungamila,  Kata  ya Kasokola, Wilaya  ya Mlele, amefariki  dunia  baada  ya kutumbukia  ndani ya ndoo ya maji  akiwa  nyumbani  kwao.
Tukio  hilo lilitokea juzi saa  10 jioni  wakati  mtoto huyo alipokuwa  akicheza  na  dada  yake,  Stella  David (5).
Wakati tukio hilo linatokea mama wa watoto hao alikuwa amekwenda mtoni kufua nguo
Chanzo:Tanzania Daima 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa