Home » » HOT NEWS: KIJANA ALA MVUA YA MIAKA 30 KWA KUMBAKA KIKONGWE

HOT NEWS: KIJANA ALA MVUA YA MIAKA 30 KWA KUMBAKA KIKONGWE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

jela  miaka 30 kwa kubaka kikongwe
 N a Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda  Mkoa wa Katavi imemuhukumu   John  Joseph  30  Mkazi wa Tarafa ya M pibwe  Wilaya ya Mlele Mkoani  hapa  kifungo cha miaka 30 jela  baada ya kupatikana na hatia ya  kumbaka kwa nguvu kikongwe mwenye umri wa miaka 65
Hukumu  hiyo ilitolewa hapo juzi na Hakimu Mkazi  Mfawidhiwa Mahakama ya Wilaya ya Wilaya ya  Mpanda Chiganga Ntengwa  baada ya mahakama kulidhika na ushahidi uliotolewa mahakamani na kuvutia hisia  za watu wengi
Awali katika kesi hiyo   mwendesha mashitaka  Godfrey  Luzabila  alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo hapo Agosti 18 mwaka jana majira ya saa 12 jioni  katika eneo la kijiji cha  Ifukutwa  Tarafa ya Kabungu wilayani  Mpanda ambako mshitakiwa alikuwa  amekwenda kufanya kazi za kibarua cha kutengeneza barabara
Anadaiwa   siku hiyo  alimwona mama huyo akiwa akipita barabarani  na ndipo mshitakiwa alimfuata mama huyo na kumvutia kwenye kichaka  pembeni ya barabara  aliyokuwa akifanya kazi mshitakiwa ya kuchimba mitaro
Mwendesha mashitaka Godfrey  aliiambia mahakama    mshitakiwa baada ya kumvutia kikongwe huyo polini  alimtaka  afanye nae tendo la ndoo kitendo   ambacho  mama huyo  hakukubaliana  nacho
Alisema  mama huyo  alimsihi  mshitakiwa  akatafute mwanamke mwingine wa kufanya nae  tendo la ndoa kwani umri wake  haulingani kabisa na umri wa  mshitakiwa John Joseph
Alisema pamoja na  maombi ya mama huyo mshitakiwa hakujali na ndipo alipomshika mama huyo na kumvua nguo kwa nguvu na kuanza kumbaka huku mama  huyo akipiga mayowe ya kuomba msaada
Mwendesha mashitaka alisema  kufuatia  mama huyo  kupiga mayowe  watuu watatu waliokuwa wakipita kwenye eneo hilo waliweza kusikia na  waliweza kwenda kichakani  na walimwona mshitakiwa akiwa  akimbaka mama huyo  na kasha mshitakiwa alivyo ona wanamsogelea alitokomea kichakani mahari kusiko julikana
Hakimu Mkazi   mfawidhi Chiganga Ntengwa akisoma  hukumu hiyo alieleza  kuwa kutokana na ushahidi uliotolewa   na upande wa  mashitaka ambao  ulileta mashahidi watatu  akiiwepo wa   daktari ambae  alithibiitisha  kuwa mama huyo alikuwa amebakwa na kuharibiwa sehemu za siri  hivyo mahakama haikuona shaka lolote kumtia mshitakiwa  hatiani
Hivyo   mahakama  imemtia mshitakiwa hatiani kwa kosa la kifungu cha sheria  namba  130 kifungu kidogo cha kwanza na chapili na kifungu  cha sheria namba 131
Alisema kutokana  na kupatikana  na makosa hayo mahakama imemuhukumu mshitakiwa John Joseph  kutumikia kifungo cha miaka 30  kuanzia  hapo juzi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa