Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkuutano Mkuu wa Mkoa
wa Katavi wa
Chama cha Chadema
umepitisha uamuzi wa
kuwavua yadhifa viongozi
wa chama hicho wa Jimbo
la Mpanda Mjini na
kumsimamisha mwenyekiti wao wa
Mkoa huu John Malack na kutuma
mapendekezo kwenye kamati kuu ya
Taifa ya chama hicho
mapendekezo ya kuwavua uanachama
madiwani wake waili wa Kata ya Makanyagio na Kashaululi
Wajumbe wa Mkutano huo mkuu
wa Mkoa wa Katavi
walipitisha maazimio hayo hapo juzi
kwenye mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Mtakatifu Maria wa Kanisa
Katoriki Jimbo la Mpanda na
uliongozwa na Makamu mwenyekiti wa Chadema wa Kanda ya
Magharibi Masanja Mussa Katambi
Viongozi hao
wameodholewa nyadhifa zao
kutokana na tuhuma
za kuwatolea kashifa viongozi wao wa Taifa kwenye mkutano
wao wa hadhara uliofanyika februali 2 kwenye viwanja
vya Maridadi Mjini hapa
Viongozi
walioondolewa kwenye nyadhifa
hizo ni Mwenyekiti wa Jimbo la Mpanda Mjini Seif Sipia
Katibu wa Jimbo hilo
joseph Mona katibu
mwenezi Godfrey Kapufi ambae wamemvua uanachama
kutokana na kudaiwa
kuiba nyaraka ya Chama
hiyo na kuisoma kwenye Mkutano
huo wa hadhara
Pia wajumbe wa Mkutano mkuu
huo walipitisha uamuzi
uliotolewa na kikao cha
mashauriano cha Mkoa
kilichoketi tarehe 22 Februari na kutowa uamuzi wa kumsimaisha mwenyekiti wao wa Mkoa wa Katavi John Malack
kwa tuhuma za kushiriki kwenye mkutano huo
ambao yeye ndiye
aliyefunga mkutano huo wa hadhara
Katibu
wa Mkoa wa Chama
hicho Almasi Ntije
aliwaeleza wajumbe wa Chama
hicho kuwa mwenyekiti huyo wa Mkoa
ataendelea kusimamishwa kufanya
shughuli za chama hicho
hadi hapo utakapo tolewa uamuzi juu yake na
kikao cha kamati kuu abacho ndicho
chenye mamlaka
A lisema
kwa upande wa
madiwani wakata ya Makanyagio
Iddi Nziguye na Diwani wa
Kata ya Kashaulili John
Matongo nao mapendekezo yao
ya kuwavua uanachama
yameisha pelekwa kwenye kamati kuu ya
chama hicho na ndicho kikao chenye mamlaka
nayo
Kwa upandea
wake Diwani wa Kata ya
makanyagio Iddi Nziguye alipohojiwa
na mwandishi wa habari hizo
kuhusiana na uamuzi wa mkutano
mkuu huo alisema kikao hicho
hakikuwa harali kwani kilikuwa
na wajumbe ambao
sio wajumbe wa kikao hicho
Alifafanua kuwa
idadi ya wajumbe walioshiriki mkutano huo walikuwa zaidi ya mia tatu wakati wajumbe harali wa
mkutano huo huwa hako
zaidi ya mia na
hamsini
0 comments:
Post a Comment