Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Baadhi ya Majengo
ya madarasa yaliyojengwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Mpanda hayajawahi kutumika tangia
yalipopo jengwa mwaka 2010 na yameanza
kuchakaa kutokana na Wizara ya Elimu mafunzo na ufundi kushindwa kupeleka wanafunzi shuleni hapo
Hayo yalielezwa
hapo juzu na Mkuu wa Shule hiyo Nyabise
Sabasi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mpanda
Paza Mwamlima alipotembelea shuleni hapo kwa lengo lakufanya ziara ya shule hiyo ya kukagua ujenzi wa
ukarabati wa shule hiyo
Alisema shule
hiyo ya wanafunzi i wasichana ya Kidato
cha tano na cha sita ambayo
inajumla ya majengo ya vyumba vya madarasa 30 ilifunguliwa mwaka wa 1986 na inakabiliwa na
changamoto mbalimbali
Alizitaja baadhi
ya changamoto hizo kuwa ni uchache
wa wanafunzi wanaopelekwa shuleni
hapo ambapo shule hiyo inauwezo wa kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita
wanafunzi 840 wakati waliopo ni 253 hari
ambayo imesababisha baadhi ya majengo ya
madarasa yaliojengwa toka mwaka 2010 kushindwa kutumika hadi sas
Changamoto
nyingine ni majengo mengi ya mabweni
licha kuwa na vitanda yako wazi kutokana na kukosa wanafunzi wa kulala
kwenye mabweni hayo
Kwa upande wake
mwanafunzi wa shule hiyo Magdalena
Yanga alimweleza Mkuu wa
Wilaya kuwa shule hiyo inakabiliwa na ukosefu wa shule hiyo kutokuwa na gari lolote la
usafiri pamoja na kutokuwa na zahanati hari ambayo inawazimu wanafunzi kuacha
masomo na kuwasindikiza hospitali pindi wanapo kuwa wameugua
Nae mkuu wa
Wilaya ya Paza Mwamlima aliwataka wanafunzi wa
shule hiyo wahakikishe wanaongeza bidii ya kusoma ili watakapo faulu vizuri waje kuisaidia Serikali hapo baadaye na
kuhusu mganga Serikal Imepangia kazi
watumishi mbalimbali wa kada ya afya hivyo watakapo lipoti mwezi ujao watapewa mganga hivyo ni vizuri uongozi wa
shule ukaandaa nyumba ya kuishi shuleni hapo kwa Daktari
Alisema mwaka jana shule hiyo ilikuwa ni ya
69 Kitaifa kwa matokeo ya kidato cha sita kwa hari hiyo
ni vizuri mwaka huu shule hiyo ikashika
nafasi za juu zaidi hata vyo wanafunzi
hao walihaidi mbele ya mkuu huyo wa Wilaya kuwa mwaka huu watashika nafasi tatu
za juu za ufaulu Kitaifa
0 comments:
Post a Comment