Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Diwani wa Kata ya
Ilunde Halmashauri ya Wilaya ya
Mlele kupitia chama cha Mapinduzi CCM Filberti Katola 49
amefariki Duani hapo juzi
wakati akisafirishwa kurudishwa
kijijini kwake Ilunde
Diwani huyo
alifariki juzi majira ya saa saba
mchana katika eneo la Kanono
Wilayani Mlele wakati
akiwa njiani alipokuwa
akirudishwa kijijni kwake baada ya kuwa
ametolewa katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda alikokuwa akitibiwa
Marehemu alilazwa
katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda kwa zaidi ya wiki mmoja baada ya
kuwa ametokea kwenye hospitali ya Sikonge iliyoko mkoani Tabara baada
ya
kuwa anasumbuliwa na maradhi mbalimbali
kwa kipindi kirefu
Ndugu wa marehemu waliamua kumuhamisha katika Hospitali ya wilaya ya
Mpanda na kumrudisha kijijini kwake kwenye kijiji cha Ilunde
baada ya kuona hari yake inazidi
kuwa mbaya siku hadi siku licha ya kuwaanapatiwa matibabu
Ndipo hapo juzi
wakati wakiwa njiani kwa kutumia usafiri
wa gari dogo walifika maeneo ya Kanono Diwani huyo
alifariki Dunia
Mazishi ya Diwani
Filberti Katola yamefanyika hapo jana
saa saba mchana katika makaburi ya kiji cha Ilunde na huhudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa Wilaya ya Mlele na madiwani wa Halmashari hiyo pamoja na mamia ya
wakazi wa Kata ya Ilunde
0 comments:
Post a Comment