Waziri mkuu Mizengo pinda akisalimiana na viongozi wa
kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa katavi hapo Jana mara baada ya
kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mjini Mpanda ambapo yupo kwa ajili ya
mapumziko ya krismasi kijijini kwake kibaoni.picha na walter Mguluchuma
*************************
Na Walter Mguluchuma Mpanda Katavi
Waziri Mkuu wa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mizengo Pinda jana mchana aliwasiri
mkoani Katavi kwa ajiri ya mapumziko ya
Krismasi na mwaka mpya na
kupokewa na mamia ya wakazi wa mji wa
Mpanda waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dokta Rajabu Rutengwae kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda
Waziri Mkuu Pinda
aliwassiri kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda majira ya saanane na nusu mchana na
kisha alikagua vikundimbalimbali vya ngoma
ya asili akiwa amefuatana na Balozi wa China Nchini Tanzania
Baada ya kugagua
vikundi hivyo vya ngoma Waziri Mkuu
Pinda alielekea kijijini kwake kata ya
Kibaoni kwa ajiri ya mapumziko ya Krismasi na mwaka mpya
Kwa mijibu wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya Mkuu wa
Mkoa wa Katavi siku ya jumanne ya tarehe 24 Desemba 2013
waziri Mkuu Pinda atatembelea na kukagua barabara inayojengwa kwa kiwango cha rami
kutoka Mpalamawe Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa hadi Kibaoni
Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi
Waziri Mkuu Pinda
katika ukaguzi huo wa barabara ya Mpalamawe
Kibaoni atakuwa ameongozana na Balozi wa China Nchini Tanzania ambapo
barabara hiyo inajengwa na kampuni ya kutoka chIna
0 comments:
Post a Comment