Monday, December 23, 2013

WAZIRI MKUU MH. PINDA AWASILI KATAVI KWA MAPUMZIKO YA KRISMASI.

kikundi cha ngoma asilia za kifipa kikitumbuiza wakati wa mapokezi ya waziri mkuu mizengo pinda hapo jana kwenye uwanja wa ndege wa mjini mpanda wakati waziri mkuualipowasili mkoani katavi kwa ajili ya mapumziko ya krismasi.picha na Walter Mguluchuma
Waziri mkuu Mizengo pinda akisalimiana na viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa katavi hapo Jana mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa mjini Mpanda ambapo yupo kwa ajili ya mapumziko ya krismasi kijijini kwake kibaoni.picha na walter Mguluchuma
*************************
Na Walter  Mguluchuma Mpanda  Katavi
Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Mizengo Pinda jana mchana aliwasiri  mkoani Katavi kwa ajiri ya mapumziko ya  Krismasi na mwaka mpya  na kupokewa  na mamia ya wakazi wa mji wa Mpanda waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dokta Rajabu Rutengwae kwenye  uwanja wa ndege wa  Mpanda
Waziri Mkuu Pinda aliwassiri kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda majira ya saanane na nusu mchana na kisha alikagua vikundimbalimbali vya ngoma  ya asili akiwa amefuatana na Balozi wa China Nchini Tanzania
Baada ya kugagua vikundi hivyo vya ngoma    Waziri Mkuu Pinda alielekea kijijini kwake  kata ya Kibaoni kwa ajiri ya mapumziko ya Krismasi na mwaka mpya
Kwa mijibu  wa ratiba iliyotolewa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi  siku ya jumanne  ya tarehe 24 Desemba  2013  waziri Mkuu Pinda atatembelea na kukagua barabara  inayojengwa kwa kiwango cha  rami  kutoka Mpalamawe Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa   hadi Kibaoni  Wilaya ya  Mlele  Mkoa wa Katavi
Waziri Mkuu Pinda katika ukaguzi huo wa barabara ya Mpalamawe  Kibaoni atakuwa ameongozana na Balozi wa China Nchini Tanzania ambapo barabara hiyo inajengwa na kampuni ya kutoka chIna

No comments:

Post a Comment