Home » » RAIA WA CHINA AFARIKI BAADA YA KUDUMBUKIA KWENYE SHIMO LA DHAHABU

RAIA WA CHINA AFARIKI BAADA YA KUDUMBUKIA KWENYE SHIMO LA DHAHABU

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Raia  mmoja wa Nchi  ya  China  Chen  Gungson mmiliki wa kampuni ya uchimbaji wa  madini ya  Got  Accdent On  Ming  Camp  amefariki dunia baada ya kutumbukia ndani ya shimo ambalo lilikuwa la mgodi wa dhahabu  katika machimbo ya dhahabu ya Ibidi Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi

Tukio hilo la kutumbukia kwenye shimo la mgodi huo na kusababisha kifo cha Raia huyo wa China  lilitokea hapo jana majira ya saa tatu na nusu asubuhi  katika  eneo hilo la Ibindi

Raia huyo wa China  alipatwa na mauti hayo wakati akiwa anakagua maeneo  ambayo  anafanyia shughuli zake za uchimbaji wa madini aina ya dhahabu  na ndipo alipoteleza na kutumbukia ndani ya shimo hilo la mgodi wa dhahabu

Baada ya kutumbukia jitihada za kumwokoa zilianza kufanywa na watumishi wenzake  wakiwemo na raia wengine saba wa Raia wa China  na  wananchi wanaofanya shughuli kwenye maeneo hayo  ambapo waliigiza kamba ndani ya shimo  ili marehemu aweze kuishika na wao waweze kumvuta kwa nje

Hata hivyo baada ya kuona kamba waliojaribu kumwokolea haija shikwa  Raia wanne wa China waliingia ndani ya shimo hilo  kwa kutumia kamba na waliweza kutoka na  marehemu huyo  na wao hawakujua kama  ameishafariki dunia na kumbiza hospitali ya Wilaya kwa kutumia gari yao Aina ya TOYOTA

Walipofika Hospitalini  walimshusha haraka haraka  marehemu  kwa kutumia machela na kwenda kumlaza katika kitanda kilichopo wodi namba moja na kuwataka wauguzi wampe huduma ndugu yao huyo ya matibabu

Mganga wa zamu Dokta Benald Mbushi  alifika kwenye wodi hiyo na alipompima  Raia huyo wa China aliwaeleza kuwa  Mchina huyo ameisha fariki  hata kabla ya kufikishwa hospitalini hapo

Kwa upande wake Dokta Benald Mbushi ameeleza kuwa mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuifadhi maiti cha hospitali ya wilaya ya Mpanda ukisubili kufanyiwa uchunguzi kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu zake

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi amethibitisha kutokea kwa kifo cha Raia huyo wa kutoka  nchi ya China  na ametowa wito kwa watu kutotembea karibu na mashimo ya migodi hasa katika kipindi hiki cha masika

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa