Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mtu mmoja Yunge Maboja (70) Mkazi wa Kijiji cha
Kapanda Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amefariki dunia
baada ya kushambuliwa na wananchi kwa kupigwa na silaha za
jadi ngumi na mateke baada ya kukutwa uchini usiku wa manane kwenye
shimo la kuchimba dhahabu na kutuhumiwa kuwa alikuwa akiroga
ili mwenye shimo hilo asipate madni ya dhahabu
Kwa mijibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishina Dhahili
Kidavashari alisema tukio hilo la kushambuliwa kwa mtu huyo lilitokea
hapo juzi majira ya saa saba usiku katika kijiji hicho cha Kapanda
Alisema wiki tatu kabla ya tukio hilo marehemu
alimuazimisha Idd Kipara shoka ambalo alikuwa
akilitumia katika shughuli zake ulinzi katika shimo la
kuchimba madini aina ya dhahabu la Juma Ngegeshi
Alieleza marehemu alianza kumtafuta mtu aliye
muazimisha shoka na ndipo siku hiyo ya tukio majira ya saa saba
usiku alipofika kwenye shimo la kuchimba dhahabu la mtu mmoja
aliyejulikana kwa jina Lmoja La Abui ambapo alichungulia ndani ya
shimo ambalo ndani yake walikuwemo watu wili wakifanya shughuli
hizo za uchimbaji wa madini
Kamanda Kidavashari alisema watu hao waliokuwa ndani ya
shimo walishitushwa na kitendo cha marehemu kuwachungulia mida hiyo
ya usiku wa manane wakiwa ndani ya shimo hivyo iliwalazimu watoke nje ya
shimo hilo la kuchimba madini ya dhahabu ndipo walipotoka na kumkuta marehemu
akiwa uchi
Alisema ndipo watu hao wawili Abui na Hassan walipoanza
kumshambulia marehemu kwa kashfa za kuwa marehemu kuwa
ni mchawi na ndio maana amefika kwenye shimo lao akiwa uchi na ndio maana
wamekuwa hawapati madini ya dhahabu kwenye shimo hilo kwa muda mrefu
Kidavashari alieleza ndipo walipoamua kumkamata huku akiwa uchi na
kuanza kumshambulia kwa fimbo na mateke na kumlazimisha
awapeleke kwa mwenyeji wake Juma Ngegeshi ili awapatie uchawi
ambao ulikua umebaki atowe uchawi uliobaki nyumbani kwake
Walipofika nyumbani kwa Juma Ngegeshi walimkuta
mkewe aitwaye Asha Shaban ambae baada ya kuwafungulia
mlango walimtaka awaonyeshe uchawi ilikuwa umebaki ndani ya nyumba
hiyo na Asha aliwajibu ndani ya nyumba yake hakuna kitu kama hicho na
hafamu kitu kama hicho na kisha alianza nae kushambuliwa kwa
fimbo usoni na mgongoni
Alieleza hari hiyo ilimfanya Asha apige mayowe ya kuomba
msaada na ndipo majirani walipofika hapo na kukuta marehemu yuko
uchi nao waliungana kuaanza kumshambulia yeye pamoja na Asha hari
ambayo ilimfanya Asha ajifungie ndani ya nyumba yake
Kidavashari alieleza majeruhi wote wawili walifikishwa kituo cha
polisi cha Mpanda na kisha walipelekwa Hospitali ya Wilaya ya
Mpanda na marehemu alilazwa kutokana na hari yake kuwa mbaya na
arifariki dunia akiwa anaendelea kupatiwa matibabu
Jitihada za kuwasaka wahusika wa tukio
zilifanyika ambapo watu wawili wanashikiliwa na jeshi
la polisi kwa mahojiano ambao ni Yunge Hassan 43
mkazi wa Mtaa ya Kashaulili na Ayub Samwel 30 Mkazi wa Kijiji cha
Kapanda na wengine wamekimbia
0 comments:
Post a Comment