Sunday, December 22, 2013

APIGWA HADI KUFA BAADA YA KUKUTWA UCHI KWENYE SHIMO LA DHAHABU

Na Walter  Mguluchuma
Mpanda  Katavi
Mtu mmoja  Yunge  Maboja  (70)  Mkazi wa Kijiji cha Kapanda  Wilaya ya Mlele  Mkoa wa Katavi amefariki  dunia  baada ya kushambuliwa  na wananchi  kwa kupigwa na  silaha za jadi ngumi na mateke  baada ya kukutwa uchini  usiku wa manane kwenye shimo la kuchimba dhahabu  na kutuhumiwa kuwa alikuwa  akiroga  ili mwenye shimo hilo asipate madni ya dhahabu
Kwa mijibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi  Kamishina Dhahili Kidavashari  alisema tukio hilo la kushambuliwa kwa mtu huyo lilitokea hapo juzi majira ya saa saba usiku  katika kijiji hicho cha Kapanda
Alisema wiki  tatu kabla ya tukio hilo  marehemu  alimuazimisha  Idd Kipara  shoka ambalo  alikuwa akilitumia  katika shughuli  zake ulinzi  katika shimo  la kuchimba madini aina ya dhahabu la Juma Ngegeshi  
Alieleza  marehemu  alianza kumtafuta  mtu aliye muazimisha  shoka  na ndipo siku hiyo ya tukio majira ya saa saba usiku  alipofika kwenye  shimo la kuchimba dhahabu  la mtu mmoja aliyejulikana kwa jina Lmoja La Abui  ambapo alichungulia ndani ya shimo  ambalo  ndani yake walikuwemo watu wili wakifanya shughuli hizo za uchimbaji wa  madini 
Kamanda Kidavashari  alisema  watu hao waliokuwa ndani ya shimo  walishitushwa  na kitendo cha marehemu kuwachungulia mida hiyo ya usiku wa manane wakiwa ndani ya shimo hivyo iliwalazimu  watoke nje ya shimo hilo la kuchimba madini ya dhahabu ndipo walipotoka na kumkuta marehemu akiwa uchi
Alisema ndipo watu hao wawili Abui  na Hassan  walipoanza  kumshambulia marehemu  kwa kashfa   za kuwa marehemu  kuwa ni mchawi na ndio maana amefika kwenye shimo lao akiwa uchi  na ndio maana wamekuwa  hawapati madini ya dhahabu kwenye shimo hilo kwa muda mrefu
Kidavashari alieleza ndipo walipoamua kumkamata huku akiwa uchi  na kuanza kumshambulia  kwa fimbo na mateke  na kumlazimisha  awapeleke kwa mwenyeji wake  Juma  Ngegeshi  ili awapatie uchawi ambao ulikua umebaki  atowe  uchawi uliobaki nyumbani kwake
Walipofika nyumbani  kwa Juma Ngegeshi  walimkuta  mkewe  aitwaye  Asha  Shaban ambae baada ya kuwafungulia mlango  walimtaka awaonyeshe uchawi  ilikuwa umebaki ndani ya nyumba hiyo na  Asha aliwajibu ndani ya nyumba yake hakuna kitu kama hicho na hafamu kitu kama hicho  na kisha  alianza nae kushambuliwa kwa  fimbo usoni na mgongoni
Alieleza hari hiyo ilimfanya Asha  apige mayowe  ya  kuomba msaada na ndipo majirani walipofika hapo na kukuta  marehemu yuko uchi  nao waliungana  kuaanza kumshambulia yeye pamoja na Asha hari ambayo ilimfanya Asha ajifungie ndani ya nyumba yake
Kidavashari alieleza majeruhi wote wawili  walifikishwa kituo cha polisi cha Mpanda  na kisha walipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Mpanda  na marehemu alilazwa  kutokana na hari yake kuwa mbaya na arifariki  dunia  akiwa  anaendelea kupatiwa matibabu
Jitihada za  kuwasaka  wahusika  wa tukio  zilifanyika  ambapo  watu wawili  wanashikiliwa  na jeshi la polisi kwa  mahojiano  ambao ni  Yunge   Hassan 43 mkazi wa Mtaa ya Kashaulili na  Ayub Samwel  30 Mkazi wa Kijiji cha Kapanda  na wengine wamekimbia

No comments:

Post a Comment