Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombelo Mkoa wa
Morogoro wamefanya ziara Katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda yenye lengo la
kujifunza namna Halmashauri hiyo ya Mji wa Mpanda
ilivyofanikiwa kuwa mshindi wa kwanza
kwa kuanza kwa mashindano ya usafi
kwa kipindi cha miaka miwili
mfulizo katika Halmashauri za Mji za hapa nchini
Ziara hiyo ya
siku mbili ya madiwani kutoka Halmashauri hiyo
ilikuwa na jumla ya madiwani
ishirini na tano na wakuu wa idara saba waliokuwa wameongozwa na makamu
mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ya Kilombelo
Ilumineta Zachalia na kaimu
mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Benson
Mihayo
Mwakamu
mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombelo aliwaelea madiwani wa Halmashauri ya
Mji wa Mpanda kwenye ukumbi wa chuo
kikuu huria cha Mkoa wa Katavi hapo juzi
kuwa lengo la ziara hiyo ni kutaka
kujifunza namna Halmashauri ya Mji wa Mpanda ilivyo fanikiwa kuwa washindi wa kwanza kwa usafi kwa kipindi
cha miaka miwili mfululizo hapa nchini
Pia alitaja lengojingine la ziara yao ni kutaka
kujifunza namna ya Mji wa Mpanda
ulivyofanikiwa kupanda hazi kutoka Halmashauri ya Mji mdogo na kuwa
Halmashauri ya mji kwa kipindi kifupi wakati wao
wanamuda mrefu hawajafanikiwa kuwa Halmashauri ya mji
Makamu mwenyekiti
huyo alisema wamevutiwa sana na namna ya Halmashauri ya mji wa Mpanda inavyofanya kazi
zake za maendeleo kwa kushirikiana na wananchi na kuufanya mji huo kukuwa kwa
kasi kubwa
Alieleza
Halmashauri ya Mji wa Mpanda imekuwa ni mfano wa kuigwa na ndio maana
Halmashauri nyingine zinakuja kujifunza kwake namna ya kufanya shughuli
mbalimbali za
kimaendeleo
Miongoni mwa
miradi waliotembelea hapa ni mradi wa chanzo cha maji ya kutega ya Iikolongo
chenye uwezo wa kuzalisha lita milioni mbili za maji kwa siku na mtambo wa kuzalisha ramani za viwanja vya
ardhi
Kwa upande wake
mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Enock Gwambasa aliwaeleza kuwa ziara
hiyo walioifanya kwenye Halmashauri yake
itakuwa na manufaa kwenye Halmashauri yao ya Kilombelo
Gwambasa alieleza
yale waliojifunza hapa Mpanda ni
vizuri wakayatumie
vizuri kwenye Halmashauri yao pindi watakapo kuwa wamwerudi kwenye
Halmashauri yao kwa munufaa ya wananchi wao

No comments:
Post a Comment