N a Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi yetu blog
Taasisi ya umoja wa Wabunge inayoshughulikia uhifadhi wa
wanyama pori na mistu
wameiomba Serikali kusimamisha
utoaji wa vibali vya vitalu kwa ajiri
ya uwindaji wa wanyama pori na
vibari vya uchimbaji wa madini
kwenye maeneo ya yanayopakana karibu na Hifadhi za Taifa kutokana
na baadhi ya makampuni hayo kutumia maeneo hayo kwa ujangili wa Tembo na
Falu
Hayo yamesemwa hapo juzi kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa
Taasisi hiyo Riziki Lulida wakati
akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Dokta Rajabu Rutengwe
ofisini kwake na wakati alipokuwa
akizunguza na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya
wanyama pori ya Katavi pamoja na
watumishi wa pori la Akiba la Rukwa Rukwaki katika chuo cha wanyama pori cha
Mlele
Lulida
alielezakuwa yapo makampuni ya kigeni ambayo yamepewa vibali vya
vitalu vya uwindaji na uchimbaji wa madini wamekuwa wakitumia vibari
hivyo vibaya na matokeo yake wamekuwa wakijihisisha na uwindaji
haramu wa Faru na Tembo hivyo ni vizuri Sekari ikasitisha walau
utoaji
wa vibali hivyo kwa kipindi cha miaka kumi
Alisema Wanyama
wetu wako hatalini kupotea na
utalii utakuwa umekufa kabisa hesabu ya mwaka 2000 inaonyesha Tanzania ilikuwa na
jumla ya Tembo milioni mbili lakini
waliopo sasa ni elfu kumi na tatu tuu
Kwaupande wake makamu mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Bunge
Mwandisi Athuman Mfutakamba alieleza
endapo hatua mahususi za haraka hazita chukuliwa utalii wan chi utakufa
na watu watakuwa wanaenda kuona wanyama kwenye nchi za wenzetu na pato letu la uchumi litapungua kwani
utalii unachangia asilimia 21 . 7 ya
pato la taifa
Alifafanua kuwa lengo la
taasisi hiyo ni pia ni kuwapa
wananchi wanaojihusisha na ujangili uwelela
wa umuhumu wa uwifadhi wa wanyama pori kwa faida za sasa na kwa siku zijazo
Aidha Katibu mkuu wa
taasisi hiyo Silvester Mabumba alieleza kuwa ni vizuri Serikali ikaongeza umakini zaidi kwa kutowaamini kupita
kiasi Raia wa kigeni kwani baadhi
yao wamekuwa wakijihusisha na ujangili
wa wanyama wetu na kuharibu mistu kwa
kujihusisha na biashara za magogo ya miti
Mkuu wa Mkoa wa Katavi
Dr Rutengwe alisema Hifadhi zetu za wanyama hazina mipaka inayo onekana hivyo
imekuwa ikichangia sana
uharibifu wa mazingira na kuongezeka kwa ujangili
Alisema ili
kukabiliana na wimbi la
ujangili lililipo kwa sasa ni muhimu
Hifahi zote zikawa na vifaa vya kisasa na mawasiliano ya uhakika
Nao watumishi wa
Hifadhi ya Katavi na wapori la akiba la Rukwa RUkwati walieleza kuwa katika
majangili wanaokamatwa katika maeneo
yao asilimia sabini ni raia wa
kigeni wa Nchi ya Burundi
Pia walieleza kuwa
wamekuwa wamekuwa wakikabiliwa na
tatizo la upungufu wa watumishi na uchache
wa magari kutokana na mbuga hiyo ya
Katavi kuwa na kilometa 4771 za mraba hivyo wanahitajika watumishi wakutosha na
magari ilikukabiliana na ujangili
0 comments:
Post a Comment