N a Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi yetu blog
Mkuu wa Kitengo
kitengo cha Dawati la unyanya wa jinsia wa
jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Mkaguzi wa wa Jeshi la polisi Viliginia
Sodoka amewataka akina baba wa Mkoani hapa kuacha tabia ya kutopeleka mashitaka yao polisi pindi wanapo
pigwa na wake zao
Sodoka alitowa
kauli hiyo hapo juzi kwenye wodi ya
wagonjwa ya wanaume wakati akizungumza na wagonjwa waliolazwa
kwenye wodi hiyo alipo watembelea na
kuwafariji ikiwa ni katika sehemu ya
siku kumi na sita ya kuhamasisha
kupinga unyanyansaji wa jinsia
Katika ziara hiyo
ya kutembelea hospitali ya Wilaya ya Mpanda
kitengo hicho kilitowa
msaada wa sabuni , biscuti na vinywaji baridi kwa wagonjwa waliolazwa katika wodi
mbalimbali vikiwa na thamani ya shilingi
laki tatu na nusu
Mkuu huyo wa
kiteno cha dawati la jinsia na
unyanyansaji wa jinsia alieleza kuwa
wapo wanaume wengi wamekuwa
wakifanyiwa vitendo vya
unyanyansaji na wake zao baadhi yao
wamekuwa wakipigwa na wake zao lakini wamekuwa wakiona aibu kwenda polisi
kufungua mashitaka
Sodoka aliwaeleza
acheni kuona kuona aibu mnapo
nyanyaswa na wake zenu dawati la
unyanyansaji wa jeshi la polisi
lipo wazi muda wote kusikiliza na
kutatua matatizo hayo ya unyanyasanji wa
kijinsia
Kwa upande
wake Mganga mkuu wa Hospital ya Wilaya
ya Mpanda Dokta Nasibu Mkongwa alishukuru msaada huo uliotolewa na kitengo
hicho cha polisi kwani kitawafariji wagonjwa kwani baadhi yao ndugu zao wako
mbali
Pia ametowa wito kwa taasisi
nyingine mkoani hapa kuiga mfano wa kitengo cha polisi cha dawati la
unyanyansaji wa kijinsia kwa msaada huo kwa wagonjwa na wao waige
mfano huo
0 comments:
Post a Comment