N a Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Mkuu wa Mkoa wa
Katavi Dokta Rajabu Rutengwe ametowa wito kwa Wakuu wa Wilaya na na
Wakurugenzi wa Halmashauri wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha
wanawashirikisha wananchi katika kupanga na kutekeleza
mipango ya maendeleo katika Wilaya zao
Wito huo aliutowa
hapo juzi wakati akiwahutubia Wananchi wa Tarafa ya usevya kwenye mkutano wa hadhara wa kwenye kilele
cha maadhimisho ya sherehe za
miaka 52 ya Uhuru zilizofanyika kimkoa katika Tarafa ya Usevya
Wilaya ya Mlele
Dokta
Rutengwe alisema Halmashauri za Mkoa wa katavi
zinatakiwa zinawashirikishe
wananchi wake katika kupanga mipango ya
maendeleo ambayo italenga
katika kumwondolea mwananchi
umasikini na ziwe tayari kupeleka
madaraka kwa mwananchi
Alieleza Halmashauri
ziwe ni vyombo harisi vya
wananchi na viwajibike kwa wananchi
katika utendaji wake wa shughuli zote ambazo zinahusu maendeleo
katika Halmashauri husika
Aidha
alieleza Vijana kama nguzo
ya rasilimali ya Taifa letu
ni vizuri wakawekewa
mikakati thabiti ya kuwainua
kielimu na kimaendeleo kwa ujumla
Endapo Haimashauri
zitawasahau vijana katika
mipango yao zitambue
kuwa zitalitumbukiza Taifa
kwenye hatari ya matukio mbalimbali kama vile wizi ,utapeli ujambazi
na kuenea kwa magonjwa kama vile Ukimwi
Pia alieleza kuwa
katika kipindi ca miaka 52 ya Uhuru Mkoa
wa Katavi umepata mafanikio katika sekta
mbalimbali za maendeleo ambazo
Alisema wakati wa Uhuru mkoa wa
Katavi ulikuwa
na shule za msingi sita na sekondari
kulikuwa hakuna shule ya
sekondari hata moja ambapo baada ya miaka 52 ya Uhuru Mkoa wa Katavi
unashule za msingi 194 na shule za Sekondari 37 na chuo kimoja cha
VETA na chuo cha maendeleo ya jamii kimoja na Serikali ipo mbioni
kuanza ujenzi wa chuo kikuu cha kilimo cha Katavi
Upande wa Afya
Mkoa una hospitali moja Vituo vya afya
kumi na tatu na zahanati zilizopo
ni 61 hali hii ni nzuri ukilinganisha na
wakati wa uhuru ilivyokuwa ambapo vituo vya Afya na zahanati havikuwepo kwenye maeneo ya
vijiji alisema DR Rutengwe
Alisema huduma ya
maji imeboreshwa ambapo wakati wa Uhuru asilimia moja ya wananchi katika mkoa
wa Katavi ndio walikuwa wakipata maji safi na salama ambapo
kwa sasa asilimia arobaini na nane
ya watu 271.010 ya wakazi wa Mkoa wa Katavi wananufaika na maji safi na salama lengo la Mkoa na Taifa kwa ujumla
ni kufikia asilimia sitini na saba
Maadhimishi ya
sherehe hizo yalitanguliwa na
upandaji wa shamba darasa namba moja la
mkoa wa Katavi la Waziri Mkuu Mizengo Pinda lililoko katika kijiji cha Kibaoni ambapo wanachi
walijifundishwa namna ya kilimo bora cha kisasa
na kupanda mbegu bora za mahindi
kwa mstali
Pia zoezi hilo la
upandaji wa mahindi liliwashirikisha viongozi mbalimbali wa Mkoa wakiongozwa na
Mkuu wa Mkoa wa na viongozi wa wilaya za
Mpanda na Mlele
0 comments:
Post a Comment