Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Raia
mmoja wa Nchi ya China Chen Gungson mmiliki wa kampuni
ya uchimbaji wa madini ya Got Accdent On Ming
Camp amefariki dunia baada ya kutumbukia ndani ya shimo ambalo lilikuwa
la mgodi wa dhahabu katika machimbo ya dhahabu ya Ibidi Wilayani Mlele
Mkoa wa Katavi
Tukio hilo la kutumbukia kwenye shimo la mgodi huo na kusababisha kifo cha
Raia huyo wa China lilitokea hapo jana majira ya saa tatu na nusu
asubuhi katika eneo hilo la Ibindi
Raia huyo wa China alipatwa na mauti hayo wakati akiwa anakagua
maeneo ambayo anafanyia shughuli zake za uchimbaji wa madini aina
ya dhahabu na ndipo alipoteleza na kutumbukia ndani ya shimo hilo la
mgodi wa dhahabu
Baada ya kutumbukia jitihada za kumwokoa zilianza kufanywa na watumishi
wenzake wakiwemo na raia wengine saba wa Raia wa China na
wananchi wanaofanya shughuli kwenye maeneo hayo ambapo waliigiza kamba
ndani ya shimo ili marehemu aweze kuishika na wao waweze kumvuta kwa nje
Hata hivyo baada ya kuona kamba waliojaribu kumwokolea haija shikwa
Raia wanne wa China waliingia ndani ya shimo hilo kwa kutumia kamba na
waliweza kutoka na marehemu huyo na wao hawakujua kama
ameishafariki dunia na kumbiza hospitali ya Wilaya kwa kutumia gari yao Aina ya
TOYOTA
Walipofika Hospitalini walimshusha haraka haraka marehemu
kwa kutumia machela na kwenda kumlaza katika kitanda kilichopo wodi namba moja
na kuwataka wauguzi wampe huduma ndugu yao huyo ya matibabu
Mganga wa zamu Dokta Benald Mbushi alifika kwenye wodi hiyo na
alipompima Raia huyo wa China aliwaeleza kuwa Mchina huyo ameisha
fariki hata kabla ya kufikishwa hospitalini hapo
Kwa upande wake Dokta Benald Mbushi ameeleza kuwa mwili wa marehemu huyo
umehifadhiwa katika chumba cha kuifadhi maiti cha hospitali ya wilaya ya Mpanda
ukisubili kufanyiwa uchunguzi kabla ya kukabidhiwa kwa ndugu zake
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi amethibitisha kutokea kwa kifo cha Raia
huyo wa kutoka nchi ya China na ametowa wito kwa watu kutotembea
karibu na mashimo ya migodi hasa katika kipindi hiki cha masika
0 comments:
Post a Comment