Home » » MADIWANI KILOMBELO WAJIFUNZA KUTOKA HALMASHAURI YA MJI WA MPANDA‏

MADIWANI KILOMBELO WAJIFUNZA KUTOKA HALMASHAURI YA MJI WA MPANDA‏

Na Walter Mguluchuma
Mpanda  Katavi
Madiwani  wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombelo Mkoa wa Morogoro wamefanya ziara Katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda yenye lengo la kujifunza  namna  Halmashauri hiyo ya Mji wa Mpanda ilivyofanikiwa  kuwa  mshindi wa  kwanza  kwa kuanza kwa mashindano ya  usafi  kwa kipindi  cha miaka miwili mfulizo katika Halmashauri za Mji za hapa nchini

Ziara hiyo ya siku mbili ya madiwani kutoka Halmashauri hiyo  ilikuwa na jumla ya madiwani  ishirini na tano na wakuu wa idara saba waliokuwa wameongozwa na makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo ya Kilombelo  Ilumineta  Zachalia na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri hiyo  Benson Mihayo

Mwakamu mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilombelo aliwaelea madiwani wa Halmashauri ya Mji  wa Mpanda kwenye ukumbi wa chuo kikuu huria cha Mkoa wa Katavi  hapo juzi kuwa lengo la ziara hiyo ni  kutaka kujifunza namna Halmashauri ya Mji wa Mpanda ilivyo fanikiwa  kuwa washindi wa kwanza kwa usafi kwa kipindi cha miaka miwili  mfululizo hapa nchini

Pia  alitaja lengojingine la ziara yao ni kutaka kujifunza  namna ya  Mji wa Mpanda  ulivyofanikiwa  kupanda hazi  kutoka Halmashauri ya Mji mdogo na kuwa Halmashauri ya mji kwa kipindi kifupi  wakati wao  wanamuda mrefu hawajafanikiwa kuwa Halmashauri ya mji

Makamu mwenyekiti huyo alisema  wamevutiwa  sana na namna ya  Halmashauri ya mji wa Mpanda inavyofanya kazi zake za maendeleo kwa kushirikiana na wananchi na kuufanya mji huo kukuwa kwa kasi kubwa

Alieleza Halmashauri ya Mji wa Mpanda imekuwa ni mfano wa kuigwa na ndio maana  Halmashauri nyingine zinakuja kujifunza  kwake namna ya kufanya shughuli mbalimbali za kimaendeleo

Miongoni mwa miradi waliotembelea hapa ni mradi wa chanzo cha maji ya kutega ya Iikolongo chenye uwezo wa kuzalisha lita milioni mbili za maji kwa siku  na mtambo wa kuzalisha ramani za viwanja vya ardhi

Kwa upande wake mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda Enock Gwambasa aliwaeleza kuwa ziara hiyo walioifanya kwenye Halmashauri yake  itakuwa na manufaa kwenye Halmashauri yao ya Kilombelo

Gwambasa alieleza yale waliojifunza hapa Mpanda  ni vizuri   wakayatumie  vizuri kwenye Halmashauri yao pindi watakapo kuwa wamwerudi kwenye Halmashauri yao kwa munufaa ya wananchi wao

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa