Home » » HOT NEWS: Walimu watatu na Mfanyabiashra jela miaka 571 kwa wizi wa milioni 21 za shule‏

HOT NEWS: Walimu watatu na Mfanyabiashra jela miaka 571 kwa wizi wa milioni 21 za shule‏

Na  Walter  Mguluchuma-Katavi yetu blog
Mahakama  ya wilaya ya Mpanda  Mkoa wa Katavi  imewahukumu  waalimu
watatu wa Shule ya Msingi  Tukoma  iliyoko  Tarafa ya Nsimbo  Wilaya
ya Mlele  Mkoa wa Katavi  na Mfanyabiashara wa Mjini  Mpanda  kifungo
cha miaka 579 jela kwa wote baada ya kupatikana na hatia ya kuiba
fedha za shule  kiasi cha  shilingi milioni ishirini  na moja
Hukumu  hiyo ilitolewa hapo jana  na Hakimu Mkazi  Mfawidhi wa
Mahakama ya Wilaya  ya Mpanda  Chiganga Ntengwa baada ya mahakama
kuwatia hatiani kwa jumla ya  makosa sitini na  nane
Washitakiwa waliohumumiwa  hapo jana ni Joel Mwakyusa (37)   Mwalimu
wa shule ya Msingi Tukoma  Mkazi wa  Kawajense  ambae amehukumiwa
kifungo cha miaka  255 baada ya kupatikana na makosa arobaini ya wizi
wa fedha, Lenatus Ngalo   (50)  mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Tukoma
 Mkazi wa Nsemlwa amehukumiwa kifungo cha miaka 148  baada ya
kupatikana na hatia ya makosa 38
Wengine waliohukumiwa ni Joachimu  Katabi  (39) Mwalimu wa shule ya
Msingi Tukoma  Mkazi wa Majengo  ambae amehukumiwa kifungo cha miaka
143 na  Fredilik  Mlenje  (50) mkazi wa  Nsemulwa  Mfanyabiashara
ambae akaunti yake  ilitumika kuibia fedha hizo  shilingi milioni 21
mali ya shule hiyo
 Washitakiwa hao  walidaiwa kutenda kosa hilo la wizi wa fedha za
shule ya  Msingi Tukoma  hapo  mwaka 2009  kwa kugushi  nyaraka ambazo
ziliwawezesha  kuiba fedha hizo kwa kupitia akaunti  ya mshitakiwa wa
nne  Fredilik Mlenje
Akisoma hukumu  hiyo iliyochukua masaa mawili  kuisoma  Hakimu Mkazi
Mfawidhi Chiganga Ntengwa  alisema  baada ya kusikiliza  mwenendo
mzima wa  kesi  mahakama yake  imewaona  wshitakiwa  wanapatikana na
makosa  kwa mujibu wa vifungu vya sheria Namba 384,335, 337,270 na 242
 Washitakiwa kabla ya kusomewa hukumu walipewa  nafasi ya kujitetea
ambapo waliomba mahahama  iwasamehe kwani kuna  familia zao
zinawategemea pamoja na wazazi  wao
Baada ya maombi hayo mwendesha mashitaka Mkaguzi wa Polisi Ally Mbwijo
alipinga maombi hayo na kuiomba mahakama itowe adhabu kali ili iwe
fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za kuiba mali ya umma
Ndipo hakimu alipowasomea washitakiwa adhabu  hiyo ya kifungo jela
kwa washitakiwa hao na kuwataka watakapo maliza kifungo hicho wote kwa
pamoja walejeshe fedha hizo mali ya shule ya Msingi Tukoma

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa