Na Walter Mguluchuma-Katavi yetu blog
Mahakama ya wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imewahukumu waalimu
watatu wa Shule ya Msingi Tukoma iliyoko Tarafa ya Nsimbo Wilaya
ya Mlele Mkoa wa Katavi na Mfanyabiashara wa Mjini Mpanda kifungo
cha miaka 579 jela kwa wote baada ya kupatikana na hatia ya kuiba
fedha za shule kiasi cha shilingi milioni ishirini na moja
Hukumu hiyo ilitolewa hapo jana na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa baada ya mahakama
kuwatia hatiani kwa jumla ya makosa sitini na nane
Washitakiwa waliohumumiwa hapo jana ni Joel Mwakyusa (37) Mwalimu
wa shule ya Msingi Tukoma Mkazi wa Kawajense ambae amehukumiwa
kifungo cha miaka 255 baada ya kupatikana na makosa arobaini ya wizi
wa fedha, Lenatus Ngalo (50) mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Tukoma
Mkazi wa Nsemlwa amehukumiwa kifungo cha miaka 148 baada ya
kupatikana na hatia ya makosa 38
Wengine waliohukumiwa ni Joachimu Katabi (39) Mwalimu wa shule ya
Msingi Tukoma Mkazi wa Majengo ambae amehukumiwa kifungo cha miaka
143 na Fredilik Mlenje (50) mkazi wa Nsemulwa Mfanyabiashara
ambae akaunti yake ilitumika kuibia fedha hizo shilingi milioni 21
mali ya shule hiyo
Washitakiwa hao walidaiwa kutenda kosa hilo la wizi wa fedha za
shule ya Msingi Tukoma hapo mwaka 2009 kwa kugushi nyaraka ambazo
ziliwawezesha kuiba fedha hizo kwa kupitia akaunti ya mshitakiwa wa
nne Fredilik Mlenje
Akisoma hukumu hiyo iliyochukua masaa mawili kuisoma Hakimu Mkazi
Mfawidhi Chiganga Ntengwa alisema baada ya kusikiliza mwenendo
mzima wa kesi mahakama yake imewaona wshitakiwa wanapatikana na
makosa kwa mujibu wa vifungu vya sheria Namba 384,335, 337,270 na 242
Washitakiwa kabla ya kusomewa hukumu walipewa nafasi ya kujitetea
ambapo waliomba mahahama iwasamehe kwani kuna familia zao
zinawategemea pamoja na wazazi wao
Baada ya maombi hayo mwendesha mashitaka Mkaguzi wa Polisi Ally Mbwijo
alipinga maombi hayo na kuiomba mahakama itowe adhabu kali ili iwe
fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hizo za kuiba mali ya umma
Ndipo hakimu alipowasomea washitakiwa adhabu hiyo ya kifungo jela
kwa washitakiwa hao na kuwataka watakapo maliza kifungo hicho wote kwa
pamoja walejeshe fedha hizo mali ya shule ya Msingi Tukoma
No comments:
Post a Comment