Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amezitaka
Halmashauri zote Nchini ambazo maeneo yao yana migodi ya madini
kuhakikisha kuhakikisha wanatowa taarifa za fedha zinazopatikana kutokana na ushuru
wa madini kwa wananchi wao
Waziri Muhongo alitowa kauli hiyo hapo
jana wakati akiwahutubia viongozi wa Mkoa wa
Katavi na wachimbaji wa madini katika mkutano uliofanyika
kwenye ukumbi Wa Idara ya maji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda wakati
wa ziara yake yasiku mbili ya kukagua miradi ya maendeleo ya Wizara hiyo
Alieleza kuwa wananchi katika maeneo mbalimbali
hapa nchini wamekuwa wakipotosha
kuwa Halmashauri zimekuwa hazipati ushuru kwenye maeneo
yao unaotokana na ushuru unaotokana na madini kitu ambacho sio
sahihi
Alisema hakikisheni mnawasomea wananchi wenu mapato
yote ambayo Halmashauri zenu zinapata kutoka kwenye
makampuni yanayochimba madini badala ya kuwaficha wananchi na
matokeo yake yamekuwa ni wananchi kujenga chuki kwa makampuni hayo wakijua kuwa
Halmashauri zao hazipati chochote kutoka kwa makampuni ya uchimbaji wa madini
Pia alizitaka Halmashauri kuhakikisha
fedha wanazolipwa kutokana na ushuru wa madini zinatumika
kwa ajiri ya shughuli za maendeleo kwenye maeneo yo
Profesa Muhongo alieleza zipo baadhi ya Halshauri
wamekuwa wakitumia pesa hizokwa ajili ya watumishi
wao kwenda kujifundisha namna ya kuzowa taka kwenyw mikoa
mingine hayo siyo matumizi mazuri ya fedha alisema Muhongo
Aidha alieleza kuwa serikali imeshaweka utaratibu
ambao hakuna mgodi ambao unaanzishwa hapa
Nchini bila kuwa na ubia na Serikali ndio utaratibu
ambao umeisha wekwa na wizara hiyo kwani kama tulikosea mwanzo
hatutakiwi kukosea tena
Pia aliwashauri wachimbaji wadogo
wadogo waanzishe vyama vyao ili iwe rahisi kwao
kukopeshwa mikopo ambayo itawasaidia kununua vifaa vya kisasa
Viongozi wa wachimbaji wawe na utaratibu wa
kuwasikiliza kero za wachimbaji vijijini kuliko ilivyo
sasa ambapo wachimbaji wanapiga simu moja kwa moja kwa waziri
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi DR Rajabu
Rutengwe alieleza kuwa mbali ya mkoa kuwa na madini mbalimbali kama vile
Dhahabu Shaba bado wachimbaji wanakabiliwa na changamoto
mbalimbali
Rutengwe alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwani
vifaa duni wanavyotumia kuchimbia na mitaji midogo kwa
wachimbaji
Nae Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo wa Mkoa wa
Katavi Willy Mbogo alimweleza waziri Muhogo kuwa jumla ya leseni 1035 zimeisha
tolewa kwa wachimbaji wadogo wa Mkoa wa Katavi
0 comments:
Post a Comment