Home » » HALMASHAURI YA MJI KUPATA BILIONI KUMI NA MBILI KWA UJENZI WA MIUNDO MBINU‏

HALMASHAURI YA MJI KUPATA BILIONI KUMI NA MBILI KWA UJENZI WA MIUNDO MBINU‏

Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi

Halimashauri ya Mji wa Mpanda inatajia  kupata shilingi Bilioni kumi na mbili kwa ajiri ya kuboresha miundo mbinu mbalimbali za Halmashauri hiyo katika Mjiwa wa Mpanda
Hayo yalisemwa hapo juzi na Mkurugenzi wa Halimashauri ya Mji wa Mpanda Selemani Lukanga kwenye kikao cha baraza la Madiwani wa Halimashauri hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu huria cha Mkoa wa Katavi
Lukanga alieleza kuwa fedha hizo shilingi Bilooni kumi na mbili  zinatolewa na Serikari kwa mkopo wa kutoka Benki ya Dunia

Alitaja miundo mbinu zitakazo tengenezwa kuwa ni  ujenzi wa soko kubwa la kisasa katika eneo la soko la zamani na ujenzi wa sitendi ya  mabasi  katika eneo la Ilembo
Aliitaja miundo mbinu mingine kuwa ni ujenzi wa barabara  zenye urefu wa kilometa saba kwa kiwango cha lami katika barabara za mjini pamoja na ujenzi wa mitalo katika mitaa mbalimbali ya mji huu

Alieleza kuwa wataalamu mbambali  wanatarajiwa kufika hivi kalibuni kwa ajili ya kuangalia maeneo hayo  kwa ajiri ya maandalizi ya awali  ya ujenzi wa miundo mbinu hiyo
Pia aliesema Halimashauri  imepanga kujenga sehemu ya kuegesha magari makubwa katika maeneo ya Misunkumilo kwa ajiri ya magari yanayo toka Mkoa wa Kigoma na Ilembo kwa ajiri ya magari yanayotoka Sumbawanga na Tabora

Alifafanua kuwa Halimashauri imeamua kujenga maeneo ya kuengesha magari ya mizigo kufuatia magari hayo kuwa yamekuwa  yakifanya uharibifu wa barabara za lami zilizopo mjini hapa na  kutokana na kuwa na uzito mkubwa na yamekuwa yakipaki  katika maeneo yasiyo lasimi kama vile kwenye nyumba za kulala wageni na matokeo yake Halimashauri imekuwa ikikosa mapato

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa