Na Walter
Mguluchuma
Mpanda Katavi
Jeshi la polisi
Mkoa wa Katavi limewakamata na kuwashikilia watu wanne kwa tuhuma za ujambazi wa
kutumia silaha haina ya SMG na kupola
pesazaidi ya shilingi milioni moja simu
na baiskel baada ya kuwapola wakazi wa Kijiji cha Ilebula Tarafa ya
Kabungu Wilaya ya Mpanda na kuwatisha
kwa kufyatua risasi hewani
Kamanda wa polisi
wa Mkoa wa Katavi Dhahiri Kidashari
aliwataja wanao shikiliwa kwa tuhumaza ujambazi kuwa ni Sengwa Moja( 43).Amosi
Ngasa (43)Barabasi Kasomi (44)na Moja Sengwa(42) wote wakazi wa kijiji cha
Ilebula B kata ya Katuma Tarafa ya
Kabungu Wilayani hapa
Alisema
watuhumiwa hao wanadaiwa mnamo
Agosti 2 mwaka huu majira ya saa
6 usiku wakiwa majqmbazi watano huku
wakiwa na silaha moja bunduki aina ya
SMG walivamia na kupola
fedha na simu za wananchi wa
kijiji hicho na wakati wanaendelea na
upolaji walifyatua risasi mbili
hewani kwa lengo la kuwatisha wananchi
Kamanda
Kidavashari alieleza baada ya
kuwatisha kwa risasi waliweza
kuwapola Juma Kubu
alipolwa pesa tsh 132,000
na simu moja aina ya Teckno yenye
thamani ya tshs 40,000 Moshi Masanilo
alipolwa baiskeli moja aina ya Abika yenye thamani ya Tshs 160,000
Alfonce Charles alipolwa pesa tshs 130.000 na simu aina ya
Xxtel ya thamani ya Tshs 65,000 Jumanne Kashindye simu moja yenye thamani ya Tshs40,000
Cristina John pesa tasilimu tshs 120,000
simu aina ya Teckno ya tshs 45.000
Sisilia Ezekiel simu aina ya
Oking ya Tshs60,000
Kamanda
Kidavashari aliwataja wengine waliopolwa kuwa ni Regina Ezekiel alipolwa
pesa tasilimu Tshs 60,000 simu aina ya Nokia Tshs 40,000 Cosmas Mathias
pesa Tshs 140 ,000 na simu ya Tsh 40,000 na Doto Peter aliye polwa simu ya Tshs
70,000 jumla ya pesa na malizote walizopola
kuwa ni kiasi cha Tshs1,240,000
Pia majambazi
hao walipola baiskeli tatu na kutoweka nazo ambapo baadae
zilipatikana zikiwa zimetelekezwa kichakani
katika eneo la shamba la gereza
la Karilankulunkulu barabara
iendayo Tarafa ya Karema
Kamanda
Kidavashari alisema katika eneo la tukio
ganda moja la risasi ya aina ya SMG liliokatwa lilihusisha
silaha iliyo tumiwa katika ujambazi huo
Alieleza Kamanda
wa Mkoa wa Katavi upelelezi unaendelea wa tukio hilo na watuhumiwa
watafikishwa mahakamani baada ya
upelelezi kukamilika
0 comments:
Post a Comment