Home » » UNHCR yatoa gari kwa mahakama

UNHCR yatoa gari kwa mahakama

SHIRIKA Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), limekabidhi msaada wa gari aina ya Toyota Land Cruiser kwa ajiri ya Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi. Msaada huo,umekabidhiwa jana na Mkuu wa UNHCR Mkoa wa Katavi, Rose Muchina.


Muchina alisema shirika lake, limeona umuhimu wa shughuli zinazofanywa na mahakama hiyo, lakini zinakwamishwa kwa sababu ya kukosa usafiri.

Alisema shirika hilo, bado linaendelea kuwahudumia wakimbizi kutoka nchini Burundi ambao wanaishi katika makazi ya wakimbiziya Katumba na Mishamo.

Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda, Chiganga Tengwa alisema msaada huo, umetolewa wakati muafaka. 

Nae Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo,Nyando Robarti alisema gari hilo litawawasaidia kuwaewzesha kufika na kutoa huduma katika maeneo ambayo hayana mahakimu wa mwanzo kama vile Karema na Mwese

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa