Na Walter
Mguluchuma
Mpanda
Kaimu wa mkuu wa Taasisi ya
kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU(PCCB)
wa Mkoa wa Katavi Cristopher Nakua
amewataka wananchi waelewe
kuwa wafanyakazi wa Taasisi hiyo wanafanya kazi zao kwa uaminifu na kwa uadilifu mkubwa
hivyo wananchi washirikiane na taasisi hiyo katika kupambana na Rushwa
Kauli hiyo aliitowa hapo jana wakati akifungua semina ya
siku moja iliyoandaliwa na Takukuru na kuwashirikisha wawakilishi wa wadau
katika nyanja zote hususani watunga sera
na sheria na watekelezaji wa sera
na kusimamia sheria iliyofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu Huria cha Mkoa wa Katavi
Washiriki wa semina walitoka katika idara zaserikali
kuu serikali za mitaa vyama vya
wafanyabiashara mashirika ya hiari taasisi za dini vyama vya siasa wanahabari
pamoja na wawakilishi wa vyama
vya wafanyakazi
Washiriki wengine wa
semina hiyo walikuwa ni Wataaluma, wakulima, wanafunzi, wazee kwa vijana watu wenye ulemavu akina pamoja naMama
Lengo la
semina hiyo ilikuwa ni kujadiliana na kubadilishana mawazo ili kuibua
maoni ya njia sahihi za kupashana habari ili kupanua wigo wa ufahamu
kuhusu Rushwa na jinsi wananchi wanavyo weza
kushiriki katika mapambano
yadhidi ya Rushwa
Kaimu Mkuu wa Takukuru
wa Mkoa wa Katavi Nakua alisema kuwa
tasisi hiyo imekuwa ikikabiliwa na tatizo wananchi kuwa na uoga
pale ambapo wanapo kuwa wakihitajika
kutowa ushahidi kuhusiana na tuhuma mbambali zinapo
kuwa zikiwakabili watu kuhusiana
na Rushwa
Alisema
wananchi wasiwe na mashaka na Takukuru hasa pale wanapo wanapo kuwa
wakiwahihaji kutowa ushahidi kwani watumishi wa Takukuru ni
waaminifu na wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili ya
kazi zao hivyo ni vizuri wananchi washiriki kwenye ushahidi pindi
wanapo kuwa
wakiitajika kutowa ushahidi
Nakua pia aliwafafanulia
malalamiko mbambali yaliyo tolewa
na washiriki wa semina hiyo likiwepo la
tatizo la kesi zinazo funguliwana Taasisi
hiyo kuchelewa kutolewa maamuzi katika mahakama mbalimbali
Aliwaeleza kuwa
kesi hizo zinachelewa kumalizika mahakamani kutokana na utaratibu uliopo kwani kesi zote wanazo zifungua kabla ya kuanza
kusikilizwa ni lazima zipelekwe kwanza
kwa Mkurugenzi wa mashika
wa hapa nchini(DPP).
0 comments:
Post a Comment