Na Walter Mguluchuma-Katavi yetu blog
Mpanda-Katavi
Jeshi la polisi mkoa wa Katavai
kwa kushirikiana na askari wa hifadhi ya Taifa ya Katavi wamewakata watu wawili
wakiwa na nyara za serikali ngozi ya chui mbili zenye thamanai ya zaidi ya
milioni 10.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa
wa Katavi kamishina msaidizi Emmanuel Nlay aliwataja waliokamatwa ni Komanya
Luponya (28) mkazi wa kijiji cha Mbede wilaya ya Mlelel na Heleni Jilala (20)
mkazi wa Muzye Sumbawanga mkoani Rukwa
Alisema watuhumiwa hao
walikamatwa Mei 22 mwaka huu majira ya saa moja asubuhi katika eneo la kijiji
cha Mwamadulu tarafa ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoa wa katavi.
Watuhumiwa hao walikamatwa
kufuatia taaraifa zilizokuwa zimelifikia jeshi la polisi kuwa watu hao
wanajihusisha na uwindaji haramu katika hifadhi ya taifa ya katavi.
Nlay alieleza polisi kwa
kushirikiana na askari wa ifadhi ya katavi walifanikiwa kuwakuta watuhumiwa wakiwa kwenye kambi
waliyofikia ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya malisho ya ng’ombe.
Baada ya kupkuliwa watuhumiwa
walikutwa na nyara za serikali ngozi mbili za chui zenye thamani ya shilingi
Tsh. 10,500,000/=
Kaimu kamanda Nlay alieleza
watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kuwa umekamilika ili
waweze kujibu mashitaka ya kukamatwa na
nyara za serikali.
0 comments:
Post a Comment