Na Walter
Mguluchuma
Mpanda
Jeshi la polisi
mkoa wa katavi lina washikilia watu
watatu kwa tuhuma za kuwakamata na Bangi
katika matukio mawili tofauti likiwemo la mtu mmoja kukamatwa na debe moja la
Bangi lenye uzito wa kilo tano.
Kaimu
kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi Emanuel Nlay alisema katika tukio la kwanza
polisi waliwakamata watu wawili David Sumun
(54) na Joseph Peter (30) wote wakazi wa kijiji cha Dilifu wilaya ya mlele
wakiwa na Bangi kete 163 zenye uzito wa Gram 815
Watuhumiwa
hao walikamatwa hapo Mei 16 Mwaka huu majila ya saa 8 mchana katika kijiji cha Dilifu kufutia msako uilio
fanywa na polisi kwa kushilikiana na sungusungu wa kijiji hicho.
Katika tukio
la pili polisi wamemkamata January Katambala (33) mkazi wa kijiji cha Mtisi
wilaya ya mlele alikamatwa akiwa na Dawa za kilevya aina ya Bangi debe moja yenye uzito wa kilo tano
kaimu
kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Emanuel Nlay alisema mtuhumiwa
alikamatwa hapo mei 25 Mwaka huu majira
ya saa 12 Jioni akiwa nyumbani kwake.
Alisema mtuhumiwa alikamatwa kufutiwa taarifa ambazo zilikuwa
zimelifikia Jeshi la hilo kuwa mtuhumiwa amekuwa akijiusisha na Biashala haramu ya kununua na
kuuza Bangi.
Baada ya
tarifa hizo polisi walianza uchunguzi na ndipo ilipo timia siku hiyo ya tukio walipo weza kufanikiwa kukamata
mtuhumiwa akiwa na Bangi hiyo aliyokuwa
amehifadhi ndani ya nyumba yake.
Nlay amesema
watuhumiwa hao wote watatu wanatarajiawa kufikishwa mahakamani wakati wowote
mara baada ya upelelezi kufanyika.
0 comments:
Post a Comment