Na Walter Mguluchuma-Katavi yetu Blog
Mpanda
Mkazi wa mtaa wa Kotazi
wilayani Mpanda mkoa wa Katavi BARAKA Mtaki (32) amejiua kwa kunywa vidonge
baada ya kupimwa afya yake na kukutwa na maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi.
Kaimu kamanda wa polisi wa mkoa
wa Katavi kamishina msaidizi Emmanuel Nlay alisema tukio hili limetokea Mei 24
mwaka huu majira ya saa 10 jioni nyumbani kwa marehemu.
Alisema siku hiyo ya tukio
marehemu Baraka alikunywa vidonge vya maralia aina ya mseto vidonge 12 na
frajili sita kwa wakati mmoja akiwa chumbani kwake.
Marehemu alikunya vidonge hivyo
baada ya mkewe aitwae Tatu Philipo (32) kuondoka nyumbani na kuelekea mashineni
kusaga unga.
Kaimu kamanda Nlay alieleza
baada ya mkewe tatu kurudi nyumbani na alipoingia ndani alimkuta marehemu akiwa
amelala huku povu likimtoka mdomoni na alipojaribu kumsemesha hakuweza
kumuitikia.
Tatu baada ya kuona hali hiyo
ilimlazimu aombe msaada kwa majirani ambao walifika katika eneo hilo
Nlay alieleza baada ya majirani
kufika hapo waliamua kumchukua marehemu na kumkimbiza katika hospitali ya
wilaya ya Mpanda wakati wakimwinua kitandani waliweza kuona pembeni alipokuwa
amelala pakiwa na paketi mbili za adawa ya maralia aina ya mseto zikiwa
zimebaki paketi tupu na vidonge sita vya Frajili vilivyokuwa vimeachwa na mkewe
navyo vikiwa paketi tupu.
Marehemu alipofikishwa katika
hospitali ya wilaya ya mpanda alifariki baada ya muda si mrefu wakati akiwa
amekwisha anza matibabu .
Kaimu kamanda alieleza hivi
karibuni marehemu alipoona anasumbuliwa
na maradhi ya mara kwa amara aliamua kwenda kupimwa afya yake na ndipo
alipokutwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Kutokana na hali hiyo marehemu
aliweza kuwaambia rafiki zake pamoja na
mkewe kuwa ktokana na kugunduliwa yeye na virusi vya ukimwi ni bora siku moja
ajiue kwa kunya vidonge kuliko kuendelea na mateso ya maradhi.
0 comments:
Post a Comment