Na Walter Mguluchuma
Mahakama
ya
Hakimu mkazi ya Wilaya ya
Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu Lyanga Chilu (70) mkazi
wa kijiji cha Kamsisi Tarafa ya Inyonga Wilayani
Mlele kifungo cha miezi mitatu jela kwa kosa la kukamatwa na
bangi miche 57
shambani kwake.
Hukumu hiyo ilitolewa hapo juzi
na Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Chiganga
Tengwa baada ya mshitakiwa kukiri kosa hilo
Awali katika
kesi hiyo iliyo fikishwa
mahamani kwa
mara ya kwanza hapo juzi mwendesha mashitaka
wa Ally Mbwijo aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa alitenda
kosa hilo Aprili 9 mwaka
huu majira ya saa 6
mchana katika kijiji cha Kamsisi
Alisema mshitakiwa alikamatwa na miche hiyo ya
bangi kufuatia taarifa zilizo kuwa
zimelifikia jeshi la polisi kuwa
mshitakiwa alikuwa akijihusisha na na
biashara ya
kuuza bangi na kuvuta
Mwendesha mashitaka baada
ya kumsomea mshitakiwa Lyanga alikiri
kupatikana na miche hiyo 57
ya bangi
Hakimu Chiganga baada ya mshitakiwa kukiri shitaka
hilo alimtaka shitakiwa kabla ya mahakama kumpa
hadhabu inampa nafasi mshitakiwa ajitee
Katika utetezi
wake mshitakiwa aliiomba
mahakama imwachie huru kutokana
na umri wake kuwa mkubwa na shughuli hiyo
ya bangi ndio aliyo kuwa
akiitegemea kumpatia kipato katika
maisha yake kwa kipindi cha
muda mrefu
Hata
hivyo utetezi huu haukuweza kukubaliwa
na mahakama baada ya mwendesha
mashitaka kupinga vikari utetezi huo kwa
kuiomba mahakama itowe adhabu kwa mshitakiwa
ili iwe fundisho kwa watu wengine
Akisoma
hukumu akimu mkazi mfawidhi Chiganga alisema
mahamani
hapo kuwa mahakama imemuhukumu mshitakiwa
Lyanga Chilu kifungo cha
miezi mitatu jela au faini ya
shilingi 70,000 mshitakiwa alishindwa
kilipa faini na amekwenda jela katika Gereza
la Mpanda
0 comments:
Post a Comment