Saturday, April 13, 2013

MZEE WA MIAKA 70 JELA MIEZI MITATU KWA KOSA LA BANGI

Na Walter Mguluchuma

Mahakama ya Hakimu  mkazi   ya   Wilaya  ya Mpanda Mkoa wa Katavi  imemuhukumu Lyanga  Chilu (70)  mkazi wa kijiji   cha Kamsisi Tarafa ya  Inyonga Wilayani Mlele  kifungo   cha  miezi   mitatu    jela   kwa   kosa   la  kukamatwa  na bangi   miche   57 shambani kwake.

Hukumu  hiyo  ilitolewa   hapo  juzi na   Hakimu  mkazi   mfawidhi  wa   mahakama     hiyo  Chiganga Tengwa  baada  ya  mshitakiwa kukiri  kosa  hilo
Awali  katika kesi   hiyo   iliyo   fikishwa mahamani   kwa mara  ya  kwanza  hapo  juzi  mwendesha  mashitaka wa Ally Mbwijo aliiambia  mahakama   kuwa  mshitakiwa  alitenda kosa hilo Aprili 9 mwaka huu   majira  ya   saa 6 mchana  katika  kijiji   cha Kamsisi
Alisema  mshitakiwa  alikamatwa  na  miche  hiyo  ya bangi  kufuatia  taarifa  zilizo  kuwa zimelifikia  jeshi  la  polisi  kuwa mshitakiwa alikuwa   akijihusisha    na   na biashara  ya kuuza  bangi  na  kuvuta  
Mwendesha  mashitaka   baada ya kumsomea mshitakiwa  Lyanga  alikiri kupatikana  na  miche  hiyo   57 ya  bangi 
Hakimu  Chiganga  baada  ya  mshitakiwa  kukiri    shitaka hilo  alimtaka  shitakiwa   kabla ya mahakama      kumpa hadhabu inampa nafasi  mshitakiwa  ajitee
Katika utetezi wake  mshitakiwa  aliiomba mahakama  imwachie  huru   kutokana na  umri  wake  kuwa  mkubwa  na  shughuli  hiyo ya  bangi   ndio  aliyo  kuwa akiitegemea  kumpatia   kipato  katika maisha  yake  kwa kipindi   cha muda  mrefu
Hata hivyo   utetezi huu  haukuweza  kukubaliwa na mahakama  baada  ya mwendesha mashitaka  kupinga  vikari  utetezi  huo   kwa kuiomba  mahakama itowe  adhabu  kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwa watu  wengine
Akisoma hukumu  akimu   mkazi  mfawidhi  Chiganga  alisema mahamani hapo   kuwa  mahakama   imemuhukumu  mshitakiwa Lyanga  Chilu  kifungo  cha miezi  mitatu  jela  au  faini  ya shilingi 70,000  mshitakiwa alishindwa kilipa  faini  na amekwenda jela katika  Gereza la Mpanda

No comments:

Post a Comment