Home » » KIZIMBANI KWA KUUA MKE NA WATOTO

KIZIMBANI KWA KUUA MKE NA WATOTO

MKAZI  wa  kijiji  cha Majimoto  wilayani Mlele  katika mkoa  wa Katavi ,Justine Albert (24)  amefikishwa  katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda  akikabiliwa  na makosa  matatu  ya  mauaji .
Justine  alifikishwa  jana (Ijumaa)  mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama  hiyo , Kiganga Tegwa  akishitakiwa  kuwaua watoto  wake wawili  ambao  ni  Justine  (6) na Eliza Justine (4)   na mama yao Jacqueline Luvika (21),.
Hata  hivyo Mshtakiwa  huyo   hakutakiwa  kujibu  lolote kwa kuwa mahakama  hiyo  haina  mamlaka  kisheria  kusilikiza  shauri hilo  ambalo  litasikilizwa katika Mahakama Kuu .
Mwendesha Mashtaka , Mkaguzi  Ally Bwijo  aliieleza mahakama  hiyo  kuwa  mshtakiwa  alitenda  ukatili  huo Aprili 06, mwaka huu  saa 11:30 alfajiri  ambapo  aliwaua  watoto  wake  hao  wawili  kisha  miili  yao  na mama yao  akiwa  hai  wakatumbukizwa katika  kisima cha maji   kijijini Majimoto .
Ilidaiwa pia  kuwa  mama  huyo aliyetumbukizwa  hai katika  kisima  cha maji  pamoja na miili  ya watoto  wake  hao  wawili kijijini humo alifariki  dunia  Aprili 07, mwaka huu katika  Hospitali  ya Wilaya  ya Mpanda  alikohamishiwa  kwa  matibabu .
Ndipo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama  hiyo , Tengwa alipolazimika  kuahirisha  kesi  hiyo Aprili 25 mwaka  huu  ambapo imepangwa  kutajwa  tena  kwa kuwa  upande  wa  mashtaka  bado  hawajakamilisha  upepelezi  wake  ila  mshtakiwa  ataamriwa kurejeshwa  rumande.
Hata hivyo kwa  mujibu wa taarifa kutoka  kijijini Majimto  pia  zimethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi , Dhahiri  Kidavashari  kulipopambazuka  siku  hiyo  ya  tukio , Aprili 06 ,mwaka huu  baadhi ya  wakazi  wa  kijiji  hicho  cha Majimoto , walio kuwa  wakienda  kwenye  shughuli  zao , waliuona  mwili wa mtoto  ukiwa  umetelekezwa  kando  ya  njia  na kumtambua  kuwa  ni Maria  mwenye umri wa  miezi  minne   ambaye ni kitinda mimba  katika familia  hiyo .
Inadaiwa wakazi hao  waliamua kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa, kumpatia taarifa hiyo huku wakiuliza mama wa mtoto aliko. Kamanda Kidavashari alidai mtuhumiwa aliwaeleza wakazi hao kuwa mama wa mtoto huyo, alikuwa ametoroka kwenda kusikofahamika na watoto wote ndipo  wakazi hao wapomtilia  shaka mtuhumiwa, wakaamua kutoa taarifa kituo cha Polisi kijijini hapo, ambao walifika ulipo mwili wa mtoto Maria wakidhani  kuwa ni  mfu .
Wakati wakiwa katika eneo la tukio, Kamanda Kidavashari alidai walibaini alama za mburuzo ardhini, wakaanza kuifuatilia na zikawafikisha kisimani. Walipofungua mfuniko wa kisima hicho, walishtuka kuona miili wa watu watatu, ikielea kwenye maji kisimani humo.
Askari Polisi kwa kushirikiana na wakazi wa kijiji hicho, waliopoa miili yote, lakini watoto hao wawili tayari walikuwa wamefariki, huku mama yao akiwa amekunywa maji mengi na kupoteza fahamu  na kukimbizwa katika Kituo  cha Afya  kijijini Mamba  kwa matibabu  lakini  alifariki  siku  iliyofuata  jioni  katika Hospitali  ya Wilaya ya Mpanda  akikohamishiwa kwa matibabu ..

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa