Na Walter MguluchumaMpanda, KataviBaadhi ya wakazi wa mitaa ya Misunkumilo na Mpanda Hotel katika mji waMpanda mkoa wa Katavi juzi waliangua vilio baada ya TANRODS mkoa waKatavi kubomoa nyumba zao zaidi ya 30 kwa ajili ya kupitisha upanuziwa barabara ya Mpanda – Kigoma ambayo inajengwa kwa kiwango cha rami.Tukio hili lilitokea kwenye mitaa hiyo hapo juzi majira ya saa 4:30asubuhi baada ya muda walio kuwa wamepewa wananchi hao kubomoa kwahiari kuwa umeishapita toka mwezi uliopita.Bomoabpmoa hiyo ya nyumba 36 ilifanyika huku kukiwa na ulinzi mkali waaskari polisi waliokuwa wameshikilia silaha kwa kile walichohofiakuwepo kwa vurugu kutoka kwa wananchi hao ambao muda wote wakati wabomoabomoa walikuwa wakiangua vilio wao na familia zao.Mmoja wa waathirika hao John Mwakapimba alisema kuwa kilicho watiauchungu zaidi ni kitendo cha nyumba zao kubomolewa bila wao kulipwafidia yoyote kwa kile walichodaiwa kuwa wao ndio waliovamia barabaraAlisema ni vema basi kabla ya kubomoa nyumba zetu serikali ingetugawiaviwanja kwanza leo hii watu waliobomolewa nyumba zao waliowengi hawanauwezo wa kujenga nyumba nyingine kutokana na umri wao kuwa mkubwa nawengine uwezo wa kifedha kuwa mdogoAlifafanua kuwa wakazi hao wa mitaa hiyo wameishakwenda kwenye maeneohayo kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 (hamsini)Wananchi wa mitaa hiyo walikuwa na mgogoro wa TANROADS mkoa wa katavitoka mwaka jana mwezi wa Novemba walipoewa notisi ya mwezi mmoja wawewamehama katika maeneo hayo ili kupitisha upanuzi wa barabara yaMpanda-Kigoma.Hata hivyo wanachi walipinga kuhama kwa kile walichodai walipwe fidiakwanza ambapo TANROADS walidai kuwa wananchi hao walilipwa malipo yaotoka mwaka 1934 ambapo walilipwa kila mmoja shilingi mia tatu kamafidia wakatiHali hiyo iliwafanya wananchi hao waombe kibali cha kufanya maandamanohapo Februari 25 mwaka huu ya kumtaka Meneja wa TANROADS Katavi IzackKamwelwe aondplewe hata hivyo Jeshi la polisi liliyafuta maandamanohayo.
Home »
» NYUMBA 36 ZABOMOLEWA, WANANCHI WAANGUA VILIO
0 comments:
Post a Comment