Home » » HATARI:MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA KATWA NA MAPANGA AKIWA AMELALA NA MWANAE WA KIKE CHUMBANI KWAKE‏

HATARI:MWANAMKE AUAWA KWA KUKATWA KATWA NA MAPANGA AKIWA AMELALA NA MWANAE WA KIKE CHUMBANI KWAKE‏


Na Walter Mguluchuma
Katavi
mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Songambele kata ya Itenka
wilayani Mlele mkoa wa Katavi Solile Juma (52) ameuwawa kwa
kukatwa katwa na mapanga wakati akiwa amelala nyumbani kwake
akiwa na mwanae kutokana na imani za kishirikina
Kaimu kamanda wa jeshi la polisi wa Mkoa wa Katavi Joseph
Myovela alisema kuwa tukio hili lilitokea hapo juzi majira ya saa
tisa usiku nyumbani kwa marehemu ambae alikuwa akiishi na
mwanae Wa kike aitwaye Nkamba Chambani (15)
Alisema siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa na mwanae huyo na
baada ya kumaliza kula mlo wa usiku waliingia kulala ambapo
mwanae alikuwa akilala sebuleni na mama yake akilala chumbani
Myovela alieleza kuwa ilipo timia majira ya saa tisa usiku
walisikia mlango ukivunjwa kwa kitu kizito na watu wasio
fahamika idadi yao waliingia ndani wakiwa na tochi zenye mwanga
mkali huku wakiongea kwa lugha ya kabila la wasukuma wakimtaka
marehemu atowe fedha zote alizo kuwa nazo
Hata hivyo marehemu huyo pamoja na mwanae hawakuweza kuwajibu
lolote watu hao kwa kuendelea kukaa kimya huku wakilazimishwa
kutopiga kelele za mayowe ya kuomba msaada kwa jirani zao
kaimu kamanda alieleza ndipo watu hao walipoanza kumshambulia
marehemu kwa kumkata kata kwa mapanga sehemu mbali mbali za mwili
wake huku mwanae akiwa akishudia tukio hilo na watu hao
wakimtaka asipige mayowe vinginevyo nayeye watamshambulia kwa
mapanga
Baada ya kuona marehemu amefariki dunia watu hao walitokomea
mahali kusiko julikana huku wakiwa hawaja chukua kitu chochote
cha marehemu Solile
Myovela alisema binti huyo wa marehemu baada ya kuona mama yake
ameuwawa aliendelea kukaa ndani hadi kuliko pambazuka ndipo
alipo chukuwa jukumu la kwenda kumtaarifu babu yake aitwaye Juma
Makoja na baada ya kufika kwenye tukio alitowa taarifa kwenye
uongozi wa kijiji ambao nao walitowa taarifa kwa jeshi la polisi
Alieleza kuwa katika tukio hili mwanae na marehemu hakujeruhiwa
sehemu yoyote ile hari ambayo inahashiria kifo hiki
kimetokana na imani za ushirikina
Hakuna mtu wala watu walio kamatwa kuhusiana na tukio hili
uchunguzi na ufuatiliaji wa kuwasaka waliohusika na mauwaji ya
haya unaendelea na mwili wa marehemu umeisha fanyiwa uchunguzi
wa daktari na wamekabidhiwa ndugu zake tayari kwa mazishi
yaliyo pangwa kufanyika jana kijijini kwake Songambele
Kaimu kamanda Myovela ametowa wito kwa wanancchi wa Mkoa wa
katavi kuepukana na imani za kishirikina ambazo zimekuwa
zikisababisha mauaji ya watu nwasiokuwa na hatia mkoani hapo

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa