Sunday, March 17, 2013

NYUMBA 36 ZABOMOLEWA, WANANCHI WAANGUA VILIO‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda, Katavi
Baadhi ya wakazi wa mitaa ya Misunkumilo na Mpanda Hotel katika mji wa
Mpanda mkoa wa Katavi juzi waliangua vilio baada ya TANRODS mkoa wa
Katavi kubomoa nyumba zao zaidi ya 30 kwa ajili ya kupitisha upanuzi
wa barabara ya Mpanda – Kigoma ambayo inajengwa kwa kiwango cha rami.
Tukio hili lilitokea kwenye mitaa hiyo hapo juzi majira ya saa 4:30
asubuhi baada ya muda walio kuwa wamepewa wananchi hao kubomoa kwa
hiari kuwa umeishapita toka mwezi uliopita.
Bomoabpmoa hiyo ya nyumba 36 ilifanyika huku kukiwa na ulinzi mkali wa
askari polisi waliokuwa wameshikilia silaha kwa kile walichohofia
kuwepo kwa vurugu kutoka kwa wananchi hao ambao muda wote wakati wa
bomoabomoa walikuwa wakiangua vilio wao na familia zao.
Mmoja wa waathirika hao John Mwakapimba alisema kuwa kilicho watia
uchungu zaidi ni kitendo cha nyumba zao kubomolewa bila wao kulipwa
fidia yoyote kwa kile walichodaiwa kuwa wao ndio waliovamia barabara
Alisema ni vema basi kabla ya kubomoa nyumba zetu serikali ingetugawia
viwanja kwanza leo hii watu waliobomolewa nyumba zao waliowengi hawana
uwezo wa kujenga nyumba nyingine kutokana na umri wao kuwa mkubwa na
wengine uwezo wa kifedha kuwa mdogo
Alifafanua kuwa wakazi hao wa mitaa hiyo wameishakwenda kwenye maeneo
hayo kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 (hamsini)
Wananchi wa mitaa hiyo walikuwa na mgogoro wa TANROADS mkoa wa katavi
toka mwaka jana mwezi wa Novemba walipoewa notisi ya mwezi mmoja wawe
wamehama katika maeneo hayo ili kupitisha upanuzi wa barabara ya
Mpanda-Kigoma.
Hata hivyo wanachi walipinga kuhama kwa kile walichodai walipwe fidia
kwanza ambapo TANROADS walidai kuwa wananchi hao walilipwa malipo yao
toka mwaka 1934 ambapo walilipwa kila mmoja shilingi mia tatu kama
fidia wakati
Hali hiyo iliwafanya wananchi hao waombe kibali cha kufanya maandamano
hapo Februari 25 mwaka huu ya kumtaka Meneja wa TANROADS Katavi Izack
Kamwelwe aondplewe hata hivyo Jeshi la polisi liliyafuta maandamano
hayo.

No comments:

Post a Comment