Home » » HALMASHAURI YASHINDWA KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI KWA KIPINDI CHAZAIDI YA MIAKA KUMI NA MOJA‏

HALMASHAURI YASHINDWA KUKAMILISHA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI KWA KIPINDI CHAZAIDI YA MIAKA KUMI NA MOJA‏


Na Walter Mguluchuma-Blogs za Mikoa
Mpanda

Wananchi wa kijiji cha  Kapanda kata ya mashimboni  wilayani Mlele  Mkoa wa  Katavi  wanakabiliwa na tatizo  la ukosefu  wa huma  ya afya  kutokana  na  kutokuwepo kwa Zahanati  kijijini hapo  kutokana  na Halmashauri  ya wilaya ya Mpanda kushindwa kukamilisha  jengo la zahanati  kwa kipindi   zaidi ya miaka  kumi  na moja.

Kutokana na  tatizo  hilo   wajumbe  wa kamati ya  ARAT  ya wajumbe wa kukagua  miradi  ya mikoa  ya Rukwa  na Katavi  ilitembelea  jengo la zahanati hiyo  hapo  novemba  mwaka jana  na kuigiza  Halmashauri  ya wilaya ya Mpanda inakamilisha  ujenzi wa jengo hilo  mapema  iwezekanavyo.

Makamu  mwenyekiti  wa ARAT wa mikoa Ya Katavi  na Rukwa  Enock  Gwambasa  jana  akiwa na wajumbe  wawili wa   walifika kijijini  hapo   ili  kukagua  ujenzi wa  zahanati hiyo   iliyo jengwa  kwa nguvu ya wananchi  kwa kushirikiana  na  hifadhi ya wanyama  pori  ya Rukwa rukwati na Halmshauri ya  wilaya ya Mpanda  iliyo pewa jukumu  la  kumalizia  hatua  ya mwisho  ya jengo la zahanati  lililoanza  kujengwa  toka mwaka 2002 ziara hiyo waliifanya hapo jana.

Gwambasa alisema   amesikitishwa na kitendo  cha  Halmashauri ya  wilaya  hiyo  kushindwa  kukamilisha  ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho  lisha  ya  kuwa maagizo yalisha tolewa.

Alieleza  hari  inaweza  ikasababisha  wahisani wanao towa  misada ya ujenzi  wa miradi  wakate tamaa  kutokana na kuchelewa kwa miradi  wanayo  saidia.

kaimu mkurugenzi  wa Halmashauri ya wilaya  ya Mpanda Justine Tibelanda  aliwaeleza wajumbe  wa kamati hiyo  ya ARAT kuwa   Halmashauri itajitahidi  kukamilisha  ujenzi wa zahanati hiyo.

 Nae  afisa mtendaji wa kata hiyo John Wambulu  alieleza  kuwa  kijiji hicho   kina  jumla  ya kaya 420  na wananchi  wamekuwa wakitembea  umbali wa  zaidi ya kilometa 20 kwenda kupata huduma  za afya  katika  zahanati ya kata  ya Magamba.

Alisema  endapo jengo la zahanati hilo  lingekuwa limekamilika   wananchi wa kijiji hicho   ambacho ni maarufu kwa uchimbaji wa dhahabu  wangeondokana  na usumbufu wa  kutembea  umbali wa muda mrefu kutafuta huduma ya  matibabu .

 kwa upande wake kaimu afisa mtendaji wa kijiji Jeturuda Kilimanjaro  alieleza kuwa  jengo hilo  limeanza kuchakaa  kutokana na wananchi kulifanyi  usafi kwa muda mrefu  na sasahizi  wamekatishwa tamaa  kuona jengo hilo  halikamiliki   na wao  kuanza  kupatiwa huduma   katika zahati ya kijiji chao. 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa