Na Walter Mguluchuma.
Mpanda.
Baraza la madiwani la Halmashauri ya mji wa mpanda mkoa wa Katavi limepitisha uamuzi wa kuitisha kikao maalumu cha daraza hilo ili kujadili tuhuma zinazo ikaibili Halmashauri hiyo inayo husuana na miradi mbambali ikiwemo ghama ya matengenezo ya shangingi la mkurugenzi wa mji huo lililo fanyiwa matengenezo kwa ghama ya shilingi milioni 40.
Uamuzi wa kuitishwa kwa kikao maalumu cha Baraza la madiwani ulipitishwa na Baraza hilo katika kikao chake kilicho fanyika desemda 31mwaka jana katika ukumbi wa chuo kikuu huria cha mkoa wa Katavi.
Taarifa ya kufanyika kwa kikao hicho ilitolewa hapo jana na mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa mpanda Enock Gwambasa alipo kuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Alisema katika kikao kilicho fanyika desemba 31 mwaka jana Baraza hilo lilishindwa kujadili taarifa ya kamati ya madiwami iliyo kuwa imepewa jukumu la kufuatilia huma za miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri yake ambayo ilikuwa na utata.
Uamuzi wa wakuitishwa kwa baraza maalumu la madiwani umezingatia ukubwa wa wa swala lenyewe la huhuma za ubadilifu wa fedha ambapo taarifa ya kamati ya madiwani wameisha kamilisha taarifa hiyo yenye kurasa 22 ili madiwani waweze kuipitia kwa kina na kuijadili.
Alifafanua kuwa kutokana na hari hiyo Baraza la madiwani waliamua kupitisha uamuzi wa kuitishwa kwa kikao maalumu cha baraza la madiwani ndani ya siku 14 baada ya kikao hicho cha desemba 31 mwaka jana.
Gwambasa alizitaja baadhi ya tuhuma za ubadilifu wa fedha ni malipo ya ya matengenezo ya gari la mkurungenzi wa Halmashauri hiyo lenye namba STK5142 aina ya shangingi lililo ghalimu matengenezo ya shilingi milioni 40 matengenezo yaliyo fanyika katika gereji inayoitwa LWICHEya mjini Sumbawanga mkoani Rukwa.
Katika malipo ya matengenezo hayo yanayo lalamikiwa kuwa ni makubwa mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa mpanda Joseph Mchina ana daiwa aliidhinisha kulipwa kwa shilingi milioni 25 za awali kwa mwenye gereji hiyo kinyume na utaratibu wa mamlaka aliyo nayo kama mkurungenzi ambapo mamlaka aliyo nayo yana mpa madaraka ya kuidhinisha malipo yanayo ishi shilingi milioni 10 tuu.
Alieleza kuwa malipo yoyote yanayo zidi shilingi milioni 10 ni lazima yaidhinishwe na kamati ya fedha na mipango utaratibu ambao hakufuatwa katika malipo hayo.
Gwambasa alizitaja huma nyingine zinazo ikabili halmashauri ya mji ni mradi wa ng’ombe wa wananchi wa kijiji cha Kakese ambapo halmashauri iliidhinisha wanunuliwe ng’ombe wakubwa lakini inadaiwa wamenunuliwa ndama kwa bei ya ng’ombe wakubwa pamoja na mradi wa ufugaji wa nguruwe katika ya kawajense.
Alitaja tuhuma nyingine kuwa madai ya ujenzi wa ghara la kuifadhia chakula katika kata ya Kakese linalo daiwa kujengwa chini ya kiwango.
0 comments:
Post a Comment