Home » » WAZEE KATAVI WAOMBA WASHIRIKISHWE KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI

WAZEE KATAVI WAOMBA WASHIRIKISHWE KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI


Na Walter Mguluchuma
Mpanda.

Umoja wa wazee wa mkoa wa Katavi wamefanya mkutano  wa kushauliana   na kubolesha  masilahi ya  wazee pamoja na kuanzisha  mfuko wao ili waweze  kuwa na dhamana  ya kupata mikopo  kwenye benki mbalimbali hapa nchini.
Mkutano huo  ulifanyika hapo  jana  kwenye ukumbi  wa  Super City   uliopo mjini Mpanda  ambao  uriwashilikisha pia  viongozi  wa  halmashauri  za mji  na wilaya  pamoja na tasisi za  fedha.
 Wazee hao  kwa pamoja  waliiomba serikari kuwaingiza wazee  katika  agenda  ya mipango  ya maendeleo  kuanzia ngazi  za   kijiji hadi taifa.
Pia walijadili changamoto  mbalimbali  zinazo wakabili   wazee hapa nchini   ambazo walizitaja kuwa ni  wazee kutokuwa  na wawakilishi    katika    vikao   vya maendeleo  na  maamuzi
Pia walidai  wanakabiliwa na  tatizo la kutokuwa na Daktarii  aliye  bobea  kwenye utaalamu  wa  kuwatibu wazee pindi wanapo kuwa wamepatwa na maradhi mbalimbali.
 Walitaja pia  walilalamikia  sera za mabenki hapa nchini  za kutowaruhusu wazee kuwakopesha mikopo  ambayo ingeweza kuwasaidia kujikimu kewnye maisha yao.
Meneja wa  benki ya  CRDB tawi la Mpanda  Selemani  Mbazi    aliwaeleza wazee hao wakati akiwasilisha maada yake kuwa  utaratibu uliopo wa mabenki  hauna utaratibu wa kuwakopesha wazee wote wenye umri wa kuanzia miaka 63
Mbazi  aliwashauri wazee hao  kuweka utaratibu  wa kuunda  vikundi  ili waweze kupata mikopo   kwani   watakuwa wameweza kutiza mashariti ya kupewa mikopo.
Kwa upande wake  katibu mkuu wa  mtandao wa  mashirika  ya wazee   tanzania  Top  Wilison  Karuwesa   alisema kwenye mkutano huo  kuwa   idadi  ya wazee  hapa nchini  kwa sasa imefikia   wazee milioni 2 na ifikapo mwaka 2050 watakuwa wamefika asilimia 10  ya wantanzania wote hapa  nchini
 Alisema  pamoja na wazee kubeba  mizigo  mizito   bado  umuhimu wao  hauja tambuliwa kwenye  jamii  na serikarini kwa ujumla.
 Miongoni mwa mizigo wanayo ibeba wazee ni kutunza yatima  ambapo asilimia 70  wanatunzwa na wazee na waathirika asilimia   80 wana tunwa na wazee pia alisema  Karuwesa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa