Home » » Uhaba wa Mahakimu tatizo Mkoani Katavi‏

Uhaba wa Mahakimu tatizo Mkoani Katavi‏


Na walter mguluchuma
Mpanda
JESHI la polisi Mkoani Katavi  limefungua jumla ya kesi 7817 za makosa  mbalimbali katika kipindi cha miaka miwili kuanzia January 2011 hadi Desemba 2012
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari kamanda  wa polisi Mkoa  wa katavi  Bw,Kidaua Shari alisema  katika kipindi hicho kulitokea  kesi nyingi ambo ni mchanganyiko.
Alisema kuwa katika kipindi  cha kuanzia januari  hadi Desemba  mwaka jana jumla ya kesi 3287 za makosa mbalimbali zilizofunguliwa  na kesi 888 ndizo zilizoweza kufikishwa mahakamani .
Hata hivyo alieleza kuwa kati ya kesi hizo zilizopelekwa mahakamani  mwaka jana ni kesi 349 ndizozilizosikilizwa na kumalizika.
Alisema mwaka 2012  kuanzia Januari hadi desemba kesi 4530 zilifunguliwa na kesi 1049 ziliweza kufikishwa  mahakamani na kesi 270 ndizo zilizoweza kusikilizwa na kumalizika.
Aliongeza kuwa katika makosa hayo makosa makubwa  ya mauaji yaliyookea  mwaka jana yalikuwa 88  na mwaka huu  makosa yalikuwa60.
Alieleza kuwa  makosa hayo makubwa yamekuwa yakisababishwa  na wizi  wa mifugo ,sababu nyingine aliiyoitoa nitamaduni  tofauti pamoja na imani za kishirikina nakuongeza kipindi cha mwaka jana makosa ya unyang’anyi yalikuwa 77 na mwaka huu ni makosa 70 yaliyofunguliwa mashitaka.
Kidaua shari  alisema kuwa kesi nyingi zinazopelekwa  mahakamani pamoja na upelelezi ukiwa umekamilika  na zile zinazochelewa kumalizika kutokana na mahakama  ya hakimu mkazi kuwa hakimu mmoja kwa Mkoa mzima.
Katika kuhakikisha  jeshi hilo limeweza kuongeza  ulinzi kwenye  minada na kwenye usafiri  wa mabasi yanayoingia na kutoka ndani ya mkoa huo wa katavi na kupunguza  matukio hayo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa