Na Walter Mguluchuma
Mpanda
SERIKALI kupitia wizara ya kilimo, chakula na ushirika imeweka mikakati ya kuhakikisha wakala wa hifadhi ya chakula YA TAIFA (NFRA) inafikia uwezo wa kuhifadhi tani 400,000 za mahindi kutoka tani 220,200 za sasa ifikapo mwaka 2014
Meneja wa NFRA mkoa wa Rukwa , Amos Mtafya alisema hayo jana wakati wa hafla fupi ya kuitimisha rasmi zoezi la uhamishaji wa mahindi tani 20,000 za mahindi lillilofanywa na askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambapo Sherehe iliyofanyika katika Kituo cha NFRA mjini Mpanda mkoani Katavi
Askari hao wa JWTZ kwa kutumia magari yao walihamisha tani hizo za mahindi kutoka maghala ya kituo cha Sumbawanga mjini na kuyapeleka mjini Mpanda mkoani Katavi ambapo zoezi hilo lilichukua siku 87.
Kwa mujibu wa Mtafya katika kutekeleza wa suala hilo , Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya China wameingia mkataba na Kampuni ya Kichina ya Jiam Gsu Muyang Gropu Co. Ltd ambayo tayari imeanza kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya mradi huo.
Aliongeza kuwa Kampuni hiyo itajenga silo katika Kanda mbalimbali nchini zitazokuwa na uwezo wa kuhifadhi tani 160,000 kwa wakati mmoja ambapo kwa Kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa imepangiwa kujengewa silo zenye uwezo wa kuhifadhi tani 20,000 za mahindi ambazo zitajengwa mijini Mpanda mkoani Katavi.
Akifafanua alisema kuwa takwimu zinaonesha miaka mitatu iliyopita kituo cha Mpanda mkoani Katavi, kimepokea chakula cha hifadhi ya tani 80,000 za mahindi kwa ajili ya kusafirishwa kwa njia ya reli ya kati wakati uwezo wa sasa wa kuhifadhi ni tani 5,000 tu ambapo ujenzi huo ukapokamilika utaweza kwa wakati mmoja kuhifadhi tani 25,000 za mahindi .
Kwa upande wake Kanali wa JWTZ, Remark Kiwovele akimwakilisha Mkuu Majeshi nchini Jenerali Devis Mwamnyange alisema kuwa zoezi hilo limesimamiwa na kuratibiwa vizuri na JWTZ ambao nao kwa upande wao wamejifunza kuishi kwa ushirikiano na Mamlaka za uraiani
Lengo la kuhamisha akiba hiyo ya chakula ni kurahisisha usafirishaji wake kwa njia ya reli kwenda mikoa ya Kanda ya kati na Ziwa ikiwemo Tabora , Dodoma,Shinyanga,Simiyu, Mwanza , Kagera na Mara ambayo mara nyingi hukumbwa na uhaba wa chakula.
0 comments:
Post a Comment