Na
Walter Mguluchuma, Mpanda – Katavi Yetu
Dereva wa kampuni ya mabasi ya Airbasi Nasibu
Ramadhani (51) amefikishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya
yam panda kwa tuhuma ya kumbaka mschana mwenye umri (13)
Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 10
mwaka huu majira ya saa 6:00 usiku katika nyumba ya kulala wageni iitwayo MIAMI
iliyopo katika mtaa wa Majengo (A).
Mwendesha mashitaka wa polisi Phinias Majula
aliiambia mahakama hiyo mbele ya Hakimu mkazi Robart Nyundo kuwa siku hiyo
Nasibu alikabidhiwa mschana huyo na wazazi wa mtoto huyo wanaoishi kijiji cha
Tutuo mkoani Tabora ili amfikishe kwa ndugu zake wanao ishi Inyonga wilayani
Mlele Mkoani Katavi.
Nasibu anadaiwa kuwa baada ya kufika Inyonga
alimpitiliza bila kumtelemsha mtoto huyo na kumsafirisha hadi wilayani Mpanda
mkoani Katavi.
Majula aliieleza mahakama kuwa baada ya
kumfikisha wilayani mpanda ambapo mtoto huyo alikuwa hajawahi kufika katika
maisha yake alipangishiwa chumba kwenye nyumba ya kulala wageni ya Miami
iliyopo mjini hapa.
Ndipo Nasibu alipomwacha mtoto huyo na kwenda
kufanya matembezi katika mitaa ya mji wa Mpanda hadi hapo majira ya usiku
aliporudi kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni na kufikia kwenye chumba
alichokuwa amemwacha mtoto huyo.
Mtuhumiwa anadaiwa baada ya kuingia ndani ya
chumba alimlazimisha mtoto huyo kufanya nae tendo la ndoa hata hivyo mtoto huyo
hakuwa tayari kufanya nae tendo hilo.
Baada ya Nasibu kukataliwa ndipo alipoamua
kutumia nguvu na kumlazimisha mtoto huyo ingawa alijitahidi kupiga kelele za
kuomba msaada hakupata msaada wowote
Majula aliendelea kuiambia mahakama kuwa
mtuhumiwa aliweza kukamatwa siku hiyo na askari waliokuwa wakifanya doria
kwenye nyumba za kulala wageni walipofikia kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni.
Ilielezwa mahakamani hapo askari wa doria walipoingia
ndani ya chumba walishitushwa na umri wa mtoto huyo na ndipo alipowaeleza mkasa
mzima wa tukio hilo.
Hakimu mkazi Robart Nyando aliamuru mshitakiwa
kwenda rumande hadi Novemba 21 baada ya mshitakiwa kushindwa kutimiza masharti
ya mdhamana
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment