Friday, November 16, 2012

DEREVA BASI KIZIMBANI KWA KUBAKAJI MTOTO WA MIAKA 13




Na Walter Mguluchuma, Mpanda – Katavi Yetu

Dereva wa kampuni ya mabasi ya Airbasi Nasibu Ramadhani (51) amefikishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi ya wilaya yam panda kwa tuhuma ya kumbaka mschana mwenye umri (13)

Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Novemba 10 mwaka huu majira ya saa 6:00 usiku katika nyumba ya kulala wageni iitwayo MIAMI iliyopo katika mtaa wa Majengo (A).

Mwendesha mashitaka wa polisi Phinias Majula aliiambia mahakama hiyo mbele ya Hakimu mkazi Robart Nyundo kuwa siku hiyo Nasibu alikabidhiwa mschana huyo na wazazi wa mtoto huyo wanaoishi kijiji cha Tutuo mkoani Tabora ili amfikishe kwa ndugu zake wanao ishi Inyonga wilayani Mlele Mkoani Katavi.

Nasibu anadaiwa kuwa baada ya kufika Inyonga alimpitiliza bila kumtelemsha mtoto huyo na kumsafirisha hadi wilayani Mpanda mkoani Katavi.

Majula aliieleza mahakama kuwa baada ya kumfikisha wilayani mpanda ambapo mtoto huyo alikuwa hajawahi kufika katika maisha yake alipangishiwa chumba kwenye nyumba ya kulala wageni ya Miami iliyopo mjini hapa.

Ndipo Nasibu alipomwacha mtoto huyo na kwenda kufanya matembezi katika mitaa ya mji wa Mpanda hadi hapo majira ya usiku aliporudi kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni  na kufikia kwenye chumba alichokuwa amemwacha mtoto huyo.
Mtuhumiwa anadaiwa baada ya kuingia ndani ya chumba alimlazimisha mtoto huyo kufanya nae tendo la ndoa hata hivyo mtoto huyo hakuwa tayari kufanya nae tendo hilo.

Baada ya Nasibu kukataliwa ndipo alipoamua kutumia nguvu na kumlazimisha mtoto huyo ingawa alijitahidi kupiga kelele za kuomba msaada hakupata msaada wowote

Majula aliendelea kuiambia mahakama kuwa mtuhumiwa aliweza kukamatwa siku hiyo na askari waliokuwa wakifanya doria kwenye nyumba za kulala wageni walipofikia kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni.

Ilielezwa mahakamani hapo askari wa doria walipoingia ndani ya chumba walishitushwa na umri wa mtoto huyo na ndipo alipowaeleza mkasa mzima wa tukio hilo.

Hakimu mkazi Robart Nyando aliamuru mshitakiwa kwenda rumande hadi Novemba 21 baada ya mshitakiwa kushindwa kutimiza masharti ya mdhamana
Blogzamikoa

No comments:

Post a Comment