Home » » DEREVA WA KAMPUNI LA MABASI LA AIR BUS ASHIKILIWA NA POLISI BAADA YA KUKUTWA KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI (GUEST) NA BINTI MWENYE UMRI WA MIAKA 13‏

DEREVA WA KAMPUNI LA MABASI LA AIR BUS ASHIKILIWA NA POLISI BAADA YA KUKUTWA KATIKA NYUMBA YA KULALA WAGENI (GUEST) NA BINTI MWENYE UMRI WA MIAKA 13‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda- Katavi.
 Dreva wa kampuni ya mabasi ya Air busi  inayo  fanya safari  zake  kutoka Tabora kuelekea Mpanda mkoa wa Katavi  Nasibu  Ramadhani   (33) anashikiliwa na jeshil la polisi wilayani  hapa kwa tuhuma za kukutwa na  mwanafunzi wa  kike  (13)  usiku akiwa amelala nae  kitanda kimoja kwenye nyumba ya kulala wageni.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa hapo jana majira   ya saa 6 usiku  katika nyumba ya kulala wageni  iitwayo  Miami  iliyoko  katika  mtaa wa majengo   wakati   polisi walipo kuwa wakifanya doria kwenye nyumba za kulala wageni.
Baada ya Nasibu  kuamshwa na mhudumu wa  gesti hiyo  ambaye  alikuwa ameambatana na polisi na ndipo  alipo ufungua mlango wa  chumba   walicho kuwa wamelala la msichana huyo.
Baada ya kuingia ndani ya chumba hicho  polisi walishikwa na butwa  kwa jinsi msichana huyo  alivyo  kuwa na umri  mdogo na alivyo weza kuwa  kwenye maeneo hayo  na mwanaume kwenye nyumba ya kulala wageni.
Hari hiyo  iliwafanya  polisi   wamfanyie maojiano msichana huyo  ambaye  alieleza kuwa yeye  ni mkazi wa  kijiji  cha  Tutuo  mkoani Tabora   wazazi wake  walimkabidhi  dreva Nasibu   ili  aweze  kusafiri nae   na amfikishe   tarafa ya Inyonga  wilayani Mlele   mkoa wa Katavi ambapo angepokelewa na ndugu  zake.
Hata hivyo baada ya kufika  Inyonga  Nasibu  alimpitiliza msichana huyo  hadi wilayani Mpanda  na   kumfikishia moja kwa moja kwenye nyumba hiyo ya kulala wageni.
Msichana huyo alieleza kuwa  baada ya kumfikishia hapo alimlazimisha walale wote na ndipo alipo weza  kumkatalia  alimlazimisha  na kumpiga makofi  na ndipo  aliweza kuzidiwa nguvu.
Alieleza  hari hiyo ilimfanya   akubaliane  na alicho kuwa akikitaka dreva huyo kwa kuhofia   usalama wake  na pia kutokana na kutokuwa na mwenyeji yoyote mjini Mpanda
 Katika maelezo yake aliyo yatowa Nasibu kwa jeshi la  polisi alieleza kuwa ilimlazimu ampitilize msichana huyo   baada ya  kutowakuta ndugu wa msichana huya katika kituo cha Inyonga.
 Jeshi la polisi  wilayani hapa limethibitisha kukamatwa  kwa mtuhumiwa na tayari taratibu za uchunguzi wa kidakitari  zimeanza  kumfanyia  uchunguzu msichana huyo.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa