Na Walter Mguluchuma
Mpanda
Umajo wa wazee wa wilaya ya mpanda mkoa wa katavi wameiomba serikali itoe Elimu ya jamii kuhusu mauwaji ya wazee kuuawa kutokana na imani za kishirikina
Kauli hiyo imetolewa na wazee hao kwenye risala yao walio isoma mbele ya mganaga mkuu wa wilaya ya Mpanda Kwenye maadhimisho ya siku ya wazee Dunia risala Ambayo ilsomwa na katibu msaidizi wa wazee hao NGANYANSA MWENDAMBALI
Walisema wazee wamekuwa wakiuwawa bila sababu kwa kile kitendao cha kuwa na umri mkubwa ndio imekuwa kigezo cha kuitwa wachawi.
Waliishukuru wizara ya Afya kwa kuanzisha kitengo cha kutoa matibabu kwa wazee ambacho kimesaidia sana kwa wazee kupata huduma kwa haraka na bila usumbufu wowote. Pia kwenye risala yao hiyo waliomba serikali iweze kutoa pensheni kwa wazee wote hapa nchini
Walisema pamoja na serikali kuwapatia huduma ya dawa bure lakini dawa bila lishe hugeuka kuwa sumu mwilini kutokana na wazee wengi kuwa na hari mbaya ya kiuchumi.
Wakielezea kufurahishwa kwao kwa huduma za matibabu wanayo patiwa katika Hospitali ya wilaya Ya Mpanda kupitia Mganga wao wa wazee Dokta PATRICK MWITA
Katika kusherekea siku hiyo ya wazee hapo jana wazee hao walifanya maandamano yaliyo anzia mtaa wa Majengo na kumalizikia katika Hospitali ya wilaya ya Mpanda.
Kwenye mandamano hayo wazee hao walikuwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali ukiwemo unao sema “Vifo vya vikongwe vitaisha lini”?
0 comments:
Post a Comment