Home » » MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA MPANDA WASUSIA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI‏

MADIWANI WA HALMASHAURI YA MJI WA MPANDA WASUSIA KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI‏


Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Madiwani wa halmashauri ya mji wa mpanda  mkoa wa katavi wamesusia kikao cha  baraza la madiwani  cha halmashauri ya mji huo  kilicho fanyika juzi  kwa kile walicho dai  kuwa mkurugenzi wao  ameshindwa kutekeleza  maazimio ya maamuzi  ya vikao vya baraza la madiwani  na matumizi mabaya  ya fedha za halmashauri hiyo na kutosimamia vizuri matumizi ya fedha za halmashauri
Kikao hicho ambacho kilifanyika juzi  katika ukumbi  wa  kanisa katoriki jimbo la mpannda  kiliongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mpanda  Enock Gwambasa na katibu wa kikao hicho alikuwa ni kaimu Mkurugenzi wa Halmashaurii hiyo Vicent Ngonyani.
Diwani wa kwanza  kuanzisha hoja hiyo  alikuwa ni diwani wa kata ya  Ilembo Wensilaus Kaputa ambaye aliomba apatiwe maelezo  ni kwanini  mkurugenzi ameshindwa kutoa taarifa  za maamuzi ya utekelezaji  wa maazimio ya vikao vya baraza hilo vilivyo fanyika tarehe  30  mwezi 11 mwaka jana na  30 machi pamoja  29 juni  na kile cha julai 23 ambavyo vilifanyika mwaka huu.
Baada ya kutolewa kwa hoja hiyo walifuata madiwani wa kata za Kashaulili  Kawajense  Makanyagio Misunkumilo  kuunga mkono hoja hizo
Miongoni mwa malamiko yaliyo daiwa na madiwani hao yako kakika idara za fedha utumishi  sheria  na idara ya kilimo
Madiwani hao  walitaka kujua taarifa ambayo ilikuwa imetolewa kwenye vikao vilivyo pita  iliyo kuwa ikieleza matumizi ya fedha yanayoonyesha  kuwa kila kata  ilipatiwa shilingi milioni 3 kwa ajiri ya shughuli za michezo  fedha ambazo  madiwani   wa kata zote tisa za halmashauri hiyo walikataa kutofika kwenye kata zao.
Ndipo walipo omba wapatiwe ufafanuzi wa fedha hizo  taarifa ambayo ufafanuzi wake hauku wekwa kwenye kikao cha juzi.
 Pia waliomba wapatiwe taarifa ya gari linalo tumiwa na mkurungenzi  wa halmashauri hiyo  lililo gharimu  matengenezo ya zaidi ya shilingi milioni 40  kwenye gereji huko sumbawanga kiwango ambacho kilipingwa na madiwani kwenye vikao vya nyuma   nayo taarifa ya maazimio  hayo hayakuwemo kwenye kikao hicho.
Vilevi walihoji   walitaka wapatiwe maelezo  kilicho sababisha  kutokuwamo kwa taarifa  kwenye baraza hilo taarifa ya kamati ya madiwani iliyo undwa kuchunguza miradi yote inayo lalamikiwa kujengwa chini ya kiwango kilicho sababisha  kamati hiyo kushindwa kufanya kazi kutokana na kutopewa ushirikiano. 
Dai jingine lililo daiwa na madiwani  ni kutokuwapo kwa majibu sahihi  ya malipo ya ng’ombe 30 walio nunuliwa na harimashauri hiyo   kwa ajiri ya vikundi vya wafugaji wa kata ya kakese ambapo malipo  yaliyo lipwa na halmashauri  kwa kila ng’ombe   ni shilingi  450,000/= kwa kila ng’ombe  mkubwa badala yake walinuliwa ng’ombe wadogo  ndokosa
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mpanda Enock Gwambasa alisema kutokana na madiwani kususia kikao hicho  amepanga kuitisha kikao cha madiwani na mkurungezi wao ili aweze kueleza  tatizo linalo sababisha kutotekelezwa kwa maamuzi ya vikao vya baraza la madiwani.
Nae Mkurugenzi wa  halmashauri ya mji wa mpanda Joseph Mchina akizungumza na Mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu akiwa mkoani Dodoma alisema yeye kwenye kikao hicho cha juzi hakuwepo wilayni mpanda
Baadhi ya vielelezo kuwa kikao cha baraza la madiwani vipo kisheria na vinapaswa kuahirishwa kwa kufuata kanuni sio mtu tu anajiamulia kuahirisha kikao
Cha msingi vikao vyote vya baraza la madiwani vinatakiwa viahirishwe kwa kufuata vifungu vya sheria vilivyoainishwa kwenye vikao vya baraza la madiwani

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa