Na Walter Mguluchuma
Mpanda.
Mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Katavi umewachagua viongozi wake watakao kiongoza chama hicho katika mkoa huo kwa kipindi cha miaka mitano
Uchaguzi huo ulifanyika juzi katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Mpanda na kusimamiwa na msimamizi mkuu wa uchaguzi huo mjumbe wa kamati kuu ya Taifa ya CCM Stephanao Wasira.
Katika mkutano huo wa uchaguzi wajumbe walimchagua Mselemu Abdala kuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi baada ya kuwashinda wapinzani wake watatu kwa kupata kura 218
Nafasi ya pili wagombe wengine wawili waliogombea nafasi hiyo ni Thomas Ngozi aliyepata kura 40 Juma Lubwe kura 9 na Mothed Mptepa kura 8
Kwa upande wa katibu mwenezi wa CCM Mkoa wa Katavi Joseph Makumbule alichaguliwa kuwa katibu mwenezi wa mkoa huop kwa kupata kura 19 dhidi ya Paulo Guyashi aliyepata kura 9
Pia Halmashauri kuu ya chama hicho mkoa wa Katavio iliwachagua Sebastiani Kapufi, Philipo Kalyalya, Beda Katani na Crisant Mwanawima kuwa wajumbe wa kamati ya siasa ya mkoa wa katavi.
Mara baada ya msimamizi wa uchaguzi kutangaza matokeo ya mshindi wa nafasi ya mwenyekit wa CCM Mkoa huo wagombe wenzake wawili walioshindwa Thomas Ngozi na Juma Lumbwe walipinga matokeo hayo kwa kile walichodai kuwa uchaguzi huo haukuwa wa haki.
Awali siku moja kabla ya uchaguzi huo wagombe hao wawili walikwenda kumlalamikia kituo cha polisi cha Mpanda mjini mgombea aliyeshinda kwa madai ya kuwachezea mchezo mchafu na kufanya ashikiliwe kwa muda katika kituo cha polisi.
0 comments:
Post a Comment