Na Walter Mguluchuma
Mpanda Katavi
Madiwani wa halmashauri ya mji wa mpanda mkoa wa katavi wamesusia kikao cha baraza la madiwani cha halmashauri ya mji huo kilicho fanyika juzi kwa kile walicho dai kuwa mkurugenzi wao ameshindwa kutekeleza maazimio ya maamuzi ya vikao vya baraza la madiwani na matumizi mabaya ya fedha za halmashauri hiyo na kutosimamia vizuri matumizi ya fedha za halmashauri
Kikao hicho ambacho kilifanyika juzi katika ukumbi wa kanisa katoriki jimbo la mpannda kiliongozwa na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mpanda Enock Gwambasa na katibu wa kikao hicho alikuwa ni kaimu Mkurugenzi wa Halmashaurii hiyo Vicent Ngonyani.
Diwani wa kwanza kuanzisha hoja hiyo alikuwa ni diwani wa kata ya Ilembo Wensilaus Kaputa ambaye aliomba apatiwe maelezo ni kwanini mkurugenzi ameshindwa kutoa taarifa za maamuzi ya utekelezaji wa maazimio ya vikao vya baraza hilo vilivyo fanyika tarehe 30 mwezi 11 mwaka jana na 30 machi pamoja 29 juni na kile cha julai 23 ambavyo vilifanyika mwaka huu.
Baada ya kutolewa kwa hoja hiyo walifuata madiwani wa kata za Kashaulili Kawajense Makanyagio Misunkumilo kuunga mkono hoja hizo
Miongoni mwa malamiko yaliyo daiwa na madiwani hao yako kakika idara za fedha utumishi sheria na idara ya kilimo
Madiwani hao walitaka kujua taarifa ambayo ilikuwa imetolewa kwenye vikao vilivyo pita iliyo kuwa ikieleza matumizi ya fedha yanayoonyesha kuwa kila kata ilipatiwa shilingi milioni 3 kwa ajiri ya shughuli za michezo fedha ambazo madiwani wa kata zote tisa za halmashauri hiyo walikataa kutofika kwenye kata zao.
Ndipo walipo omba wapatiwe ufafanuzi wa fedha hizo taarifa ambayo ufafanuzi wake hauku wekwa kwenye kikao cha juzi.
Pia waliomba wapatiwe taarifa ya gari linalo tumiwa na mkurungenzi wa halmashauri hiyo lililo gharimu matengenezo ya zaidi ya shilingi milioni 40 kwenye gereji huko sumbawanga kiwango ambacho kilipingwa na madiwani kwenye vikao vya nyuma nayo taarifa ya maazimio hayo hayakuwemo kwenye kikao hicho.
Vilevi walihoji walitaka wapatiwe maelezo kilicho sababisha kutokuwamo kwa taarifa kwenye baraza hilo taarifa ya kamati ya madiwani iliyo undwa kuchunguza miradi yote inayo lalamikiwa kujengwa chini ya kiwango kilicho sababisha kamati hiyo kushindwa kufanya kazi kutokana na kutopewa ushirikiano.
Dai jingine lililo daiwa na madiwani ni kutokuwapo kwa majibu sahihi ya malipo ya ng’ombe 30 walio nunuliwa na harimashauri hiyo kwa ajiri ya vikundi vya wafugaji wa kata ya kakese ambapo malipo yaliyo lipwa na halmashauri kwa kila ng’ombe ni shilingi 450,000/= kwa kila ng’ombe mkubwa badala yake walinuliwa ng’ombe wadogo ndokosa
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa mpanda Enock Gwambasa alisema kutokana na madiwani kususia kikao hicho amepanga kuitisha kikao cha madiwani na mkurungezi wao ili aweze kueleza tatizo linalo sababisha kutotekelezwa kwa maamuzi ya vikao vya baraza la madiwani.
Nae Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa mpanda Joseph Mchina akizungumza na Mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu akiwa mkoani Dodoma alisema yeye kwenye kikao hicho cha juzi hakuwepo wilayni mpanda
Baadhi ya vielelezo kuwa kikao cha baraza la madiwani vipo kisheria na vinapaswa kuahirishwa kwa kufuata kanuni sio mtu tu anajiamulia kuahirisha kikao
Cha msingi vikao vyote vya baraza la madiwani vinatakiwa viahirishwe kwa kufuata vifungu vya sheria vilivyoainishwa kwenye vikao vya baraza la madiwani
No comments:
Post a Comment