Na Walter Mguluchuma
Mpanda.
Maktaba ya wilaya ya Mpanda mkoa wa katavi imepatiwa msaada wa Computer tatu zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 5 kutoka kwa kampuni ya tumbaku ya TLTC
Msaada huo umekabidhiwa hapo jana mbele ya Mkuu wa wilaya yam panda Pazza Mwamlima kwenye ofisi ya Maktaba ya wilaya hiyo na mwakilishi wa Kampuni ya TLTC mkoa wa Katavi Emmanuel Shija.
Shija alieleza kuwa msaada huo wa Komputa tatu umegharimu jumla ya shilingi milioni 5, 560,000/=
Akikabidhi msaada huo mwakilishi wa Kampuni TLTC mkoa wa katavi alisema kuwa msaada huo ni sehemu ya michango mbalimbali ambayo imekuwa ikitolewa na Kampuni ya TLTC.
Kwa upande wake Mkutubi wa mkoa wa Katavi Julias Toza alimweleza mkuu wa wilaya hiyo kuwa maktaba hiyo inakabiliwa na ukosefu wa vitendea kazi vya kisasa.
Pia ina uhaba mkubwa wa machapisho ya vitabu vya shule za msingi na sekondari ambapo wanafunzi wake ndio watumiaji wakubwa wa maktaba hiyo.
Changamoto nyingine aliitaja kuwa ni udogo wa jengo la maktaba ukilinganisha na mahitaji yanavyoongezeka kielimu kwa watu kutafuta habari na mawasiliano.
Nae mkuu wa wilaya yam panda Pazza Mwamlima alisema serikali kwa upande wake inapenda sana kushirikiana na Makampuni na taasisi mbalimbali katika kuwaletea wananchi maendeleo kwa ujumla
Pia aliyaomba makampuni yanayofanya kazi za uzalishaji na wananchi wasipende kuangalia faida tuu bali wawe na tabia ya kuangalia na kujali mahali tumbaku zinakozalishwa.
Aidha alieleza kuwa maktaba ziache tabia ya kufanyta kazi kimazoea na badala yake wabuni mifumo mipya.
Vile vile alizitaka halmashauri ziangalie namna ya kuwavuta watu ili wajenge mazoea ya kujisomea kwenye maktaba kwani watanzania walio wengi hawapendi kujisomea alisema Pazza Mwamlima.
0 comments:
Post a Comment