Na Walter Mguluchuma
Mpanda – Katavi
Wakazi wa Wilaya ya Mpanda na Mlele Mkoa wa Katavi wameingiwa na hofu ya kuanza kula mlo mmoja kwa siku kutokana na kupanda kwa kasi bei ya mahindi.
Hofu hiyo imewajia kufuataia kupanda ghjafla kwa bei ya mahindi mwishoni mwa wiki iliyopita katika masoko mbalimbali ya wilaya ya Mpanda na Mlele.
Wakazi hao wakiongea kwa nyakati tofauti walisema kuwa mwanzoni mwa mwezi huu walikuwa wakiuziwa debe moja katika masoko ya mji wa mpnada kwa bei ya sh. 8000 kwa debe.
Ambapo kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita debe moja lilipanda hadi kufikia bei ya sh. 12,000/= bei ambayo haijawahi kuuzwa katika miaka ya hivi karibuni.
Mmoja wa wakazi wa mji wa Mpanda Said Ndalama alisema kutokana na kuwa na uwezo wa kipato kidogo upo uwezekana mkubwa kwa wananchi kukabiliana na ongezeko hilo la bei hari ambayo itawafanya wawe wanakula mlo mmoja kwa siku.
Alisema sababu iliyosababisha kupanda kwa bei ya mahindi ni kutokana na wakulima wengi wakati wa msimu wa mavuno kuuza mazao yao bila kujiwekea akiba.
Sababu nyingine ni walanguzio ambao wamekuwa wakifika kwa wingi kutoka katika Mikoa ya Shinyanga, Mwanza na Mara kununua mahindi na kupeleka huko.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mlele Kanali Ngemela Lubinga alisema yeye alishitushwa sana ana wananchi wake wakati wa kipindi cha kiangazi walivyo kuwa wakiuza mahindi kwa kasi kubwa.
Hali ambayo ilifanya wakati wa ziara yake kwenye tarafa mbalimbali kuwashauri wasiuze chakula chote kwa walanguzi bali wauze kile cha ziada.
Nae mkuu wa wilaya ya mpanda Paza Mwamlima alisema bei ya mahindi inapokuwa imepanda anayefurahia ni muuzaji na sio mlaji.
Alisema nivizuri msimu huu wakulima wakaongeza uzalishaji
0 comments:
Post a Comment