Home » » WAKULIMA WA TUMBAKU WAZUIWA KUFANYA MAANDAMANO

WAKULIMA WA TUMBAKU WAZUIWA KUFANYA MAANDAMANO

Na walter mguluchuma, Mpanda-Katavi Yetu
Maandamano yaliyo pangwa kufanyika jana ya wakulima wa chama cha msingi  cha wakulima  wa tumbaku  cha mpanda kati yameshindikana kufanyika.
Maandamano hayo  yameshindwa kufanyika kufuatia wakulima hao wa tumbaku  kunyimwa kibali cha kufanya  maahdamano baada ya kunyimwa kibali na jeshi la polisi.
Wakulima hao wakikuwa wameomba kibali cha kufanya maandamano yenye lengo ya kukishinikiza chama chao cha  msingi cha ushirika wa tumbaku kiwalipe malipo yao ya mauzo ya tumbaku wakio uza kwa msimu huu ulioanza mwanzoni mwa  mwezi mei  na ulimalizika mwezi agosti mwaka huu
Maandamano hayo walikuwa wamepanga yaanzie kwenye ofisi za chama chao cha msingi zilizopo katika mtaa wa kawajense kupitia kwa afisa ushirika wa wilaya ya mpanda ambaye wanamlamikia kuwa ameshindwa kusimia chama chao na kuishia  ofisini kwa mkuu wa wilaya ya mpanda.
Mmoja wa wakulima hao seif bakari alisema wameona ni bora wafanye maandamano ya kushinikiza malipo yao baada ya viongozi wao kutowapa majibu ya ukweli  mara kwa mara.
Chama hicho cha ushirika kina kabiliwa na tatizo la wakulima wake kutorosha tummbaku na kwenda kuuzia kwenye vyama vingine na hari hiyo huenda ikasabisha washindwa kulipwa malipo yao kwa asilimia mia moja.
Blogzamikoa

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Katavi yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za Mikoa