Na walter mguluchuma, Mpanda-Katavi Yetu
Maandamano yaliyo pangwa kufanyika jana ya wakulima wa chama cha msingi cha wakulima wa tumbaku cha mpanda kati yameshindikana kufanyika.
Maandamano hayo yameshindwa kufanyika kufuatia wakulima hao wa tumbaku kunyimwa kibali cha kufanya maahdamano baada ya kunyimwa kibali na jeshi la polisi.
Wakulima hao wakikuwa wameomba kibali cha kufanya maandamano yenye lengo ya kukishinikiza chama chao cha msingi cha ushirika wa tumbaku kiwalipe malipo yao ya mauzo ya tumbaku wakio uza kwa msimu huu ulioanza mwanzoni mwa mwezi mei na ulimalizika mwezi agosti mwaka huu
Maandamano hayo walikuwa wamepanga yaanzie kwenye ofisi za chama chao cha msingi zilizopo katika mtaa wa kawajense kupitia kwa afisa ushirika wa wilaya ya mpanda ambaye wanamlamikia kuwa ameshindwa kusimia chama chao na kuishia ofisini kwa mkuu wa wilaya ya mpanda.
Mmoja wa wakulima hao seif bakari alisema wameona ni bora wafanye maandamano ya kushinikiza malipo yao baada ya viongozi wao kutowapa majibu ya ukweli mara kwa mara.
Chama hicho cha ushirika kina kabiliwa na tatizo la wakulima wake kutorosha tummbaku na kwenda kuuzia kwenye vyama vingine na hari hiyo huenda ikasabisha washindwa kulipwa malipo yao kwa asilimia mia moja.
Blogzamikoa
No comments:
Post a Comment