Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi Yetu
Mashindano ya michezo ya polisijamii yaliyoshirikisha michezo mbalimbali yamemalizika jana katika uwanja wa azimio na na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa mji wa Mpanda.
Mashindano hayo yalishirikisha mchezo wa mpira wa miguu, mpira wa mikono , kukimbia mbio mita 100 kwa watu wazima, kuvuta kamba na kukamata kuku.
Katika mchezo wa mpira wa mguu timu ya Mpanda United ilifanikiwa kuwa washindi wa kwanza baada ya kuifunga timu ya polisi katavi magoli mawili kwa moja katika mchezo mkali wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 za mchezo.
Timu hiyo iilikabidhiwa kikombe pamoja na fedha taslimu tsh. 200,000 ambapo timu ya polisi katavi ilishika nafasi ya pili na kukabidhiwa ngao pamoja na fedha taslimu tsh. 150,000/= na timu ya migazini ilishika nafasi ya tatu baada ya kuifunga timu ya Lafamilia 1-0 katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu na imejipatia fedha taslimu sh. 100,000/= jumla ya timu 10 zilishiriki mashindano hayo.
Kwa upande wa mpira wa mikono timu ya polisi katavi iliibuka msindi wa kwanza na kupata zawadi ya fedha tsh. 150,000/= na timu ya katavi sitalikje walikuwa washindi wa pili na kupata sh. 100,000/=
Kwa upande wa kuvuta kamba timu ya vetelani waliwashinda timu ya polisi na kupata zawadi ya creti moja la soda na kwa upande wa mbio za mita 100 kamanda wa polisi wa mkoa wa katavi alikuwa kivutio baada ya kumaliza mashindano akiwa mshindi wa pili.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment