Wachezaji wa timu za mpira wa miguu za Uwanja wa ndege na migazini FC wakisalimiana kabla ya kuanza mchezo wao wa ufunguzi wa mashindano ya ligi ya polisi jamii Mkoa wa katavi uliofanyika katika uwanja wa Azimio mabapo timu hizo zilitoka sare ya kufungana goli moja kwa moja mashindano hayo yanajumrisha jumla ya timu nane na yalifunguliwa katika uwanja wa azimio na Mkuu wa wilaya ya mpanda Paza Mwamlima. Picha na Walter Mguluchuma
Mkuu wa wilaya mpanda Paza Mwamlima watatu kulia mwenye suti ya bluu akiwa na viongozi wa jeshi la polisi wa wilaya ya mpanda na mkoa wa katavi wakiangalia kwa makini mchezo wa mpira wa miguu wa ufunguzi wa mashindano ya rigi ya polisi jamii mkoa wa katavi mchezo uliofanyika katika uwanja wa azimio baina ya timu za uwanja wa ndege na migazini FC ambapo matokeo ya timu hizo zilitoka sare ya moja kwa moja. Picha na Walter Mguluchuma
Na Walter Mguluchuma, Mpanda-Katavi Yetu
Mashindano ya ligi ya mprira wa miguu ya polisijamii yanayozishirikisha timu nane yameanza katika uwanja wa azimio na kufunguliwa na mkuu wa wilaya yam panda Paza Mwamlima
Katika mchezo wa ufunguzi timu za Airport na migazini FC zilipambana na matokeo timu hizo zilitoka sale ya kufungana goli moja kwa moja.
Mchezo wa leo ni baina ya Katavi worriors na Lafamilia katika uwanja huo huo wa azimio mjini mpanda.
Timu ambazo zinashiriki mashindano ya polisijamii mjini hapa ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya shilingi 250,000= mshindi wa pili 200,000 na mshindi wa tatu atapata sh. 150,000 timu zinazoshiriki ni Airport FC , Migazini FC Lafamilia AF, Katavi worrirs, Makanyagio FC, Mpanda United, Kagera FC na Polisijamii.
Mbali ya mashindano ya mpira wa miguu pia kuna mashindano ya mpira wa mikono kwa wanawake na siku ya mwisho ya kilele 7/9/2012 litafanyika Bonanza la michezo mbalimbali kama vile mbio, kuvuta kamba, kufukuza kuku,bao na mpira wa miguu kwa wazee.
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment